SHARJAH YATOA TUZO KATIKA NYANJA YA HOTEL NA BANDARI YA MTWARA

DSC_0940Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Nchini Sharjah Falme za kiarabu, DR Rashid Al Leem akikabidhi tuzo ya heshima kwa Mkurugenzi wa Naf Beach Hotel, Shaibu Mohamed (SHEBBY MIX) Kwa jinsi
alivyowekeza katika sekta ya Hotel Mkoani Mtwara
DSC_0999Dr Rashid akikabidhi tuzo kwa kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Capt Husein Kasuguru baada ya kuridhishwa na kazi zinazoendelea
katika utanuzi wa Bandari hiyo

Na Abdulaziz Video,Mtwara

Serikali ya Sharjah UAE yafurahishwa na ukuaji wa Uchumi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kunakotokana na upatikani wa Nishati ya Gesi na
Mafuta na Madini na kuchangia Wananchi wengi kujitokeza kuwekeza
Katika sekta mbalimbali ikiwemo hotel za kisasa

Akiongea na glob hii, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ambae pia
anashughulikia uwekezaji katika Nchi ya Sharjah Falme za kiarabu, Dr
Rashid Al Leem aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi Tuzo ya
Umahiri kwa uwekezaji katika Sekta ya Hotel kwa Mfanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara anaemiliki Hotel za Naf Blue,Fun City na Hotel mpya ya Naf Beach Hotel Bw Shaibu Mohamed (Shebby Mix) baada ya kuridhishwa na huduma zinazotolewa alipo lala katika hotel hiyo juzi

Dr Rashid alieleza kuwa Nchi yake imeamua kuja kuwekeza katika mikoa hiyo ili kuchangia Uchumi wa wananchi wa kipato cha chini ambapo pia aliridhidshwa na ukarabati unaoendelea wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara ili kuongeza ufanisi na Huduma kwa mikoa ya kusini na Nchi Jirani ambapo pia alikabidhi tuzo kwa Meneja wa Bandari hiyo

Kukuwa kwa uchumi wa mikoa hiyo kunaendana na uwepo wa usafirishaji wa uhakika wa mizigo Kutoka na kuingia katika bandari hiyo na kuwataka wawekezaji wengine kujitokeza katika uwekezaji wa katika biashara za hotel, Uuzaji wa Umeme na kuimarisha viwanda vidogo na Ujengaji wa viwanda vikubwa kutokana na uwepo wa nishati ya Gesi na madini katika mikoa hiyoDSC_0926Naye Mmiliki wa Naf Beach Hotel alieleza kufurahishwa kwake na kupewa kwa tuzo hiyo toka Falme za kiarabu na kuhaidi kuboresha zaidi hotel zake ikiwa pamoja na kuwa karibu katika kusaidia huduma za kijamii na kuiomba Serikali hiyo kujenga utamaduni wa kutembelea mikoa ya Kusini ikiwa pamoja na kuongeza Uwekezaji na kusaidia katika nyaja ya utalii kutokana na uwepo wa vivutio Vingi

Katika ziara hiyo Dr Rashid aliambatana na ujumbe toka serikali ya
Sharjah pamoja na Balozi wa Comoro Nchini ambapo awali alitembelea
kukagua Ujenzi wa kiwanda cha Saruji Lindi, Kukagua hali ya barabara mbalimbali na kumalizia kwa kupata taarifa na kukagua Bandari ya Mtwara

BAADHI YA MANDHARI YA HOTELI YA NAF BEACH

DSC_0898Vyumba vizuri vilivyonakshiwa kwa ustadi wa hali ya juuuDSC_0977

DSC_0982Chumba Cha mikutano kikiwa na vifaa vya kisasa kabisaDSC_0953

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post