RAIS KIKWETE ATEMBELEA KITUO CHA AFYA BAGAMOYO (IHI)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Advocatus Kakorozya akimwelezea jinsi tasisi inavyotumia teknologia kupata taarifa mbalimbali za afya ambazo zimesaidia sana serikali kutunga sera.

Rais Jakaya Kikwete jana (Jumatano) alitembelea kituo cha Bagamoyo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) na kuonyeshwa kazi mbalimbali za utafiti zinazofanyika kituoni hapo. Raisi Kikwete aliisifia taasisi hiyo kwa kufanya kazi kubwa hasa katika upande wa ugonjwa wa Malaria na kujipatia sifa kubwa duniani.GovellaRais Kikwete akimsikiliza mtafiti wa IHI Dk Nico Govella akimpa maelezo juu ya utafiti wake ambapo magunia ya katani yakichanganywa na kemikali fulani yanaweza kutumika kukinga wanadamu dhidi ya mbu wanaoeneza malaria.GraceRais Kikwete akimsikiliza Grace Mwangoka wa IHI akimweleza shughuli mbalimbali za maabara kwenye taasisi hiyo.JosephRais Kikwete akimsikiliza Joseph Madata ambaye ni mkutubi akimwelezea matumizi ya maktaba mtandao (digital library) ya taasisi hiyo.GroupRais Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa IHI pamoja na wenzao kutoka Equatorial Guinea ambao wapo kwenye kituo hicho cha Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post