MKUU WA WILAYA YA KILWA AMETOA ONYO KALI DHIDI YA WAHARIBU MISITU

OFISI YA WILAYA KILWAUongozi wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi umeonya vikali dhidi ya
vitendo viovu vya baadhi ya wakulima wanaovamia misitu ya asili
iliyotengwa kwa ajili ya hifadhi ya hifadhi ya na badala yake
kuendesha kilimo cha ufuta.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega ametoa onyo hilo wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua
kuhusu ukubwa wa wa uharibifu wa misitu uliosababishwa na uvunaji
holela wa miti kwa ajili ya mbao, magogo, mkaa na kilimo cha cha ufuta wilayani humo.

clip_image002Ulega amesema pamoja na wilaya yake kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwadhibiti wavunaji holela wa mazao ya misitu, bado wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa kufuatia kuibuka kwa wimbi la wakulima wa zao hilo la ufuta kuvamia hata misitu iliyotengwa kwa ajili ya hifadhi kutokana na bei nzuri ya msimu uliopita ambayo ilifikia shilingi 2500 kwa kilo.

Amesema kutokana na bei hiyo kubwa ya mwaka jana, watu wengi
wamejiunga na kilimo hicho cha ufuta bila kushurutishwa jambo ambalo limeanza kuleta hofu ya kutokea uharibifu mkubwa wa mazingira kila mwaka na hasa kutokana na kilimo cha kuhamahama.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post