Unknown Unknown Author
Title: MABADILIKO YA MAAFISA UHAMIAJI WA MIKOA, WILAYA NA VITUO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA UHAMIAJI TAARIFA KWA UMMA YAH: MABADILIKO YA MAAFISA UHAMIAJI...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

IDARA YA UHAMIAJI

TAARIFA KWA UMMA

YAH: MABADILIKO YA MAAFISA UHAMIAJI WA MIKOA, WILAYA NA VITUO.

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, amefanya mabadiliko katika safu ya Maafisa Uhamiaji wa Mikoa, Wilaya na Wafawidhi wa Vituo mbalimbali nchini

Katika mabadiliko hayo Kamishna Mkuu Ambokile amewateua, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Jacob Sambai aliyekuwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara kuwa Msaidizi wa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara na nafasi yake inachukuliwa na Naibu Kamishna Barikieli Shayo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Kamishna wa Uhamiaji Augustino Haule ametuliwa kuwa Afisa Uhamiaji wa Mkoa Morogoro.

Mabadiliko pia yamefanyika kwa Vitengo vya Makao Makuu,Wafawidhi wa Vituo pamoja na Maafisa Uhamiaji wa Wilaya. Katika mabadiliko hayo Naibu Kamishna Hilgaty Shauri aliyekuwa Mdhibiti wa Pasipoti Makao Makuu anakuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kinondoni na nafasi yake kuchukuliwa na Naibu Kamishna Abuu Mvano ambae kabla ya mabadiliko hayo alikuwa ni Mfawidhi wa kituo cha Uhamiaji katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), wakati Naibu Kamishna Safina Muhindi ameteuliwa kuwa Afisa Uhamiaji wa Wilaya Kinondoni. Wengine ni Naibu Kamishna Fredrick Kiondo aliyekuwa Mfawidhi Kituo cha Holili anayekuwa Mfawadhi KIA, wakati nafasi yake inachukuliwa Naibu Kamishna Estomih Urio ambae kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Afisa Uhamiaji Wilaya ya Karatu. Naibu Kamishna Apolinary Msuya ameteuliwa kuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Karatu akitokea Ofisi ya Uhamiaji Tarakea Mkoani Kilimanjaro. Naibu Kamishna Evarist Mlay kutoka Tunduma anahamia Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi yake inachukuliwa Naibu Kamishna Alphonce Kwikubya aliyekuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kinondoni akisaidiwa na Naibu Kamishna Lusarago Mreka kutoka Makao Makuu.

Naibu Kamishna Sipora Moshi aliyekuwa Mfawidhi Kituo cha Bandari ya Dar es Salam ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Ubalozi Makao Makuu ya Uhamiaji na nafasi yake inachukuliwa na Naibu Kamishna Harride Mwaipyana aliyekuwa Ofisi ya Uhamiaji Kabanga. Wakati huo huo

Mabadiliko hayo ambayo yanaanza mara moja ni sehemu ya kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji ndani ya Idara ya uhamiaji katika kuwahudumia wananchi, kuwezesha uingiaji na utokaji wa watu pamoja na udhibiti wa wageni nchini. Akizungumzia mabadiliko hayo, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya, alieleza kwamba Idara imeandaa mkakati wa maboresho ya kitaasisi, rasilimali watu pamoja na vitendea kazi ili kuhakikisha kwamba watumishi wanaondokana na utendaji wa mazoea.

“Katika kulifanikisha hilo,” anasema Naibu Kamishna Irovya, “Idara ya uhamiaji imeandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao utazinduliwa hivi karibuni kwa nia ya kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa. Mkataba huo utawapatia pia wadau wa huduma za uhamiaji fursa ya kufahamu haki zao, wajibu walionao katika kupata haki hizo na mfumo mzima wakutoa mrejesho kuhusu kuduma wanazopata’’.

Mabadiliko hayo yanakuja katika kipindi cha mwezi mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amteue Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylverster Ambokile kuongoza Idara ya Uhamiaji, akichukua nafasi ya Magnus Ulungi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

MAKAO MAKUU YA IDARA IDARA YA UHAMIAJI.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top