Unknown Unknown Author
Title: HUYU NDIO MGONJWA ANAEISHI KWA MASHINE MASAA 24 KWA MIAKA 45
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Paulo Henrique Paulo Henrique Machado, raia wa Brazil ameishi hospitalini kwa kipindi cha miaka 45 sasa kutokana na kupooza kulikosaba...
clip_image002 
Paulo Henrique
Paulo Henrique Machado, raia wa Brazil ameishi hospitalini kwa kipindi cha miaka 45 sasa kutokana na kupooza kulikosababishwa na ugonjwa wa polio alioupata baada ya kuzaliwa na mama yake kufariki.

Paulo na watoto wengine walipatwa na ugonjwa huo baada ya kutokea mlipuko nchini humo miaka ya 70, na tangu wakati huo, Paulo amekuwa akipumulia mashine saa 24 kwa siku, huku watoto wenzake wengi wakiaga dunia miaka michache baadaye. 
Pamoja na masaibu mengi aliyoyapitia, yote hayo hayajawa kikwazo cha kumzuia Paulo kutumia ubongo, na akili yake kwani ameweza kupata elimu na kubobea katika masuala ya utengenezaji vikaragosi/vibonzo kwa kutumia kompyuta (computer animator) na sasa ameanza kutengeneza tamthiliya kuhusu maisha yake inayotokana na kitabu kilichoandikwa na rafiki yake --ambaye pia ni mgonjwa, Eliana-- ambayo itaonekana kwenye runinga.

Anatamani sana angeweza kucheza soka kama watoto wengine, lakini kwa kajikubali kuwa haiwezekani, ameweza kutumia akili yake kuwaza (imagination) na kufurahia mchezo huo na mengineyo.






About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top