kukutana watumishi wa Umma katika wilaya hiyo,Wengine kutoka kushoto ni kaimu Afisa elimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw Reubern Mfune
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya kutoka kata 9 za Tarafa ya Ruangwa walipokuta na mkuu wa wilaya
Na Abdulaziz Video-Ruangwa Wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wakuu hao kwa watumishi wengine wa Kada za Chini na kusababisha kuzorota kwa utendaji wa kazi hali inayosababisha jamii kutopata huduma ipasavyo na kuichukia Seikali yao.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Agnes Hokororo katika kikao cha mwisho kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa halmashauri baada ya kukamilisha kukutana na watumishi mbalimbali wa Umma wa halmashauri hiyo
Baadhi ya watumishi hasa wa idara ya elimu walilalamikia vitendo
vinavyofanywa na wakuu wa vitengo na wa idara kuwanyanyasa kwa lugha chafu hata mbele ya wanafunzi hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha maendeleo Hususan katika Kada ya ualimu.
Hokororo alisema kuwa jukumu la viongozi ni kuwa karibu na wale
waliochini yao na kuonesha ushirikiano na ili kuleta ufanisi katika
eneo la kazi na si kuonesha vitendo vya unyanyasaji.
Alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Reuben Mfune
kufuatilia tuhuma hizo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa na tabia za kuwanyanyasa walio chini yao
“Ded hakika tulikuwa wote kwenye mikutano hii na umesikia mwenyewe watumishi walivyokuwa wanasema Fanyia kazi na ndio lengo la kufikia na kupata matokeo bora sasa Imenisikitisha sana kusikia unyanyasi wa wakubwa wa Idara”, Alimalizia Hokororo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Reuben Mfune aliahidi kufanyia kazi malalamiko hayo ya watumishi hao na kuwataka watumishi hao kuendelea na majukumu yao kwa lengo la kufikia ufanisi.
Aidha Mfune alieleza kuwa Halmashauri yake imejipanga kutatua kero za watumishi ikiwemo vitendea kazi, malazi na Malipo ya usumbufu na Likizo na kuhimiza watumishi hao kutekeleza wajibu wao ili kuimarisha Wilaya hiyo inayokuwa kiuchumi.
Katika ziara hizo Mkuu wa wilaya aliweza kukutana na watumishi walio katika kata zote 21 za Wilaya hiyo hivi karibuni.
Tags
HABARI ZA KITAIFA