Unknown Unknown Author
Title: COLOMBIA: KUFUZU KWENDA BRAZIL KOMBE LA DUNIA KWALETA MAAFA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHEREHE za Nchi ya Colombia kufuzu kwenda Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1998 zimegeuka kuwa maafa...
clip_image001[6]SHEREHE za Nchi ya Colombia kufuzu kwenda Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1998 zimegeuka kuwa maafa baada ya Mashabiki watano huko Bogota, Colombia kufariki Dunia.
Juzi, Los Cafeteros, kama inavyoitwa Timu ya Taifa ya Colombia, ilicheza na Chile na kutanguliwa Bao 3-0 hadi Mapumziko lakini Kipindi cha Pili Bao la Carlos Carmona na Penati mbili za Radamel Falcao ziliwapa Colombia Sare ya Bao 3-3 na kuungana na Argentina kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia toka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini huku wakiwa na Mechi moja mkononi.
Timu 4 za juu za huko Marekani ya Kusini hufuzu kwenda Brazil moja kwa moja na ile itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenda kucheza Mechi ya Mchujo na na Timu kutoka Kanda ya Asia, ambayo ni Jordan, kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
Lakini furaha ya Mashabiki ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 16 zilizua tafrani, vurugu, ugomvi na vifo.
Kwa mujibu wa ripoti toka kwa Wanausalama, Watu watano walikufa Mji Mkuu wa Colombia, Bogota, huku watatu wakipigwa risasi na wawili kufa kwa ajali za Gari  na kutokea ripoti za Watu ‘ngumi’ zaidi ya 2,000.
Polisi wamesema Mjini Bogota Madereva 106 wa Magari walikamatwa kwa kuendesha huku wakiwa wamelewa.
MSIMAMO:

-ZIMESHAFUZU: Argentina & Colombia

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Argentina 15 9 5 1 33 12 21 32
2 Colombia 15 8 3 4 25 12 13 27
3 Ecuador 15 7 4 4 19 14 5 25
4 Chile 15 8 1 6 27 24 3 25
5 Uruguay 15 6 4 5 22 23 -1 22
6 Venezuela 16 5 5 6 14 20 -6 20
7 Peru 15 4 2 9 16 25 -9 14
8 Paraguay 15 3 3 9 16 29 -13 12
9 Bolivia 15 2 5 8 16 29 -13 11

MECHI ZA MWISHO:

[Saa za Bongo]

Jumatano Oktoba 16

02:30 Paraguay v Colombia

02:30 Chile v Ecuador

02:30 Uruguay v Argentina

05:15 Peru v Bolivia

SOURCE: SOKA IN BONGO







About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top