CAPITAL ONE CUP: MAN UNITED YAICHAPA NORWICH CITY 4–0, CHELSEA IKIFUNGA 2- 0 ARSENAL

oneMCHELSEA imeitwanga Arsenal waliokuwa kwao Emirates Bao 2-0 na kutinga Robo Fainali ya CAPITAL ONE CUP pamoja na Manchester United ambao waliwatandika Norwich City Bao 4-0 Uwanjani Old Trafford.

Timu nyingine ambazo zimetinga Robo Fainali baada ya kushinda ni West Ham na Licester City.

clip_image001Mechi kato ya Birmingham na Stoke City ilikuwa Sare ya Bao 3-3 katika Dakika 90 na ikaingia kwenye Dakika 30 za Nyongeza na Matokeo yake yakawa sare tena ya 4-4 na kufanya kupigwa kwa mikwaju ya penati na STOKE CITY KUIBUKA MSHINDI KWA PENATI 4 – 2.

ARSENAL 0 CHELSEA 2clip_image001[4]

Arsenal wakiwa kwao Emirates wamepigwa Bao 2-0 na Chelsea na kutupwa nje ya Capital One Cup.

Bao za Chelsea zilifungwa na Azpilicueta katika Dakika ya 25 na Juan Mata kwenye Dakika ya 66.

VIKOSI:

Arsenal: Fabianski; Jenkinson, Vermaelen, Koscielny, Monreal; Ramsey, Wilshere, Rosicky, Cazorla, Ryo; Bendtner

Akiba: Viviano, Sagna, Hayden, Yennaris, Ozil, Giroud, Park.

Chelsea: Schwarzer; Azpilicueta, Cahill, David Luiz, Bertrand; Essien , Mikel; De Bruyne, Mata, Willian; Eto’o

Akiba: Blackman, Ivanovic, Kalas, Ramires, Hazard, Torres, Ba.

Refa: Phil Dowd.

MAN UNITED 4 NORWICH CITY 0clip_image001[7]

Bao za Javier Hernandez ‘Chicharito’, Bao mbili, moja likiwa la Penati baada ya Januzal kuchezewa rafu, Phil Jones na Fabio, zimewapa Man United ushindi wa Bao 4-0 walipoichapa Norwich City Uwanjani Old Trafford.

Ushindi huu umeipeleka Man United Robo Fainali ya Capital One Cup.

VIKOSI:

Manchester United: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Vidic, Buttner, Zaha, Cleverley, Jones, Young, Januzaj, Hernandez.

Akiba: Amos, Anderson, Rooney, Giggs, Smalling, Fabio and Valencia.

Norwich: Bunn; Whittaker, R. Bennett, Bassong, Garrido; Snodgrass, Fer, Johnson, Redmond; Hoolahan; Elmander

MATOKEO:

Jumanne Oktoba 29

Arsenal 0 Chelsea 2

Birmingham 4 Stoke 4 [Penati 2 - 4]

Burnley 0 West Ham 2

Leicester 4 Fulham 3

Man Utd 4 Norwich 0

CAPITAL ONE CUP

RAUNDI YA 4

RATIBA

[Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku]

Jumatano Oktoba 30

Newcastle v Man City

Tottenham v Hull   

Jumatano Novemba 6

Sunderland v Southampton

<<DROO YA ROBO FAINALI KUFANYIKA JUMATANO USIKU!!>>

TAKWIMU KWA HISANI YA SOKA IN BONGO

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post