Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Mkoa wa Lindi wakihudhuria kikao cha Mkoa na kutoa Tamko kwa Chama cha Mapinduzi kuhusia na Uuzwaji wa zao la korosho
Katibu wa siasa na Uenezi Ccm,Nape Nnauye akihutubia mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana mkoa wa Lindi lililofanyika katika Ukumbi wa PEC Kilwa
Kamanda wa Vijana wa CCM Mkoa wa Lindi ambae pia ni Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe alipokuwa akitoa elimu kwa vijana kuhusiana na Rushwa ikiwemo kujiendeleza kielimu ili wanufaike na rasilimali za mkoa huo
Wadau wa ccm wilayani kilwa toka Makondeko Bar nao walihudhuria ufunguzi wa baraza hilo
Na Abdulaziz Lindi
Baraza kuu la Umoja wa Vijana mkoa wa Lindi lililokutana jana wilayani Kilwa Mkoani Lindi Llimekitaka Chama cha Mapinduzi kupitia Kamati kuu kutoa mrejesho wa maamuzi yake ya kuitaka Serikali kushughulikia tatizo la Ununuzi wa zao la korosho ikiwemo kuporomoshwa kwa Bei ya zao hilo na wajanja wachache
Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana mkoa wa Lindi, Amir Mkalipa mbele ya Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi ambae Pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Nape Mnauye katika kikao cha baraza hilo Mgeni Rasmi akiwa Kamanda wa Vijana mkoa wa Lindi (Mnec) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe
Kufuatia Tamko Hilo la Baraza kuu la Vijana Mkoa wa Lindi, Katibu wa
Uenezi, Nape Mnauye alitoa kauli ya Chama kuhusiana na tatizo hilo na
Kuwataka watakao Shindwa kutekeleza agizo hilo kwa Upande wa Serikali Kuachia Ngazi ili Chama kisihukumiwe na Wakazi wa Mikoa ya Kusini kutokana na zao hilo
“Nawahakikishia wajumbe wa Baraza kuu Chama cha Mapinduzi kupitia kamati kuu tayari kilishafanya maamuzi na kwa kuwa serikali ipo kimya sasa ifikie hatua ya Viongozi wa Serikali akiwemo waziri mkuu na waziri wa kilimo wawajibike kabla ya chama akijawajibishwa na wapiga kura” alimalizia Nape
Kwa Upande wake Kamanda Wa Vijana wa CCM, Waziri Membe alitumia Fursa hiyo kuwataka Vijana mkoani humo kutoa msukumo kwa Vijana wenzao kujikita katika kujiendeleza kielimu ili kuendana na Kasi ya Upatikanaji wa Rasilimali za Gesi, Madini na Mafuta huku akisisita Vijana kutorubuniwa na Rushwa za aina zozote ili kuepusha Migogoro ndani ya Chama
Nae Mwakilishi wa Vijana kutoka Mkoa wa Mtwara ambae aliungana na Vijana wa Mkoa wa Lindi Licha ya kufurahishwa na Tamko la Vijana hao kwa Chama cha Mapinduzi na Serikali huku akisisitiza uwepo wa Kongamano la vijana wa mkoa wa lindi na mtwara kujadli hali ya maendeleo ya mikoa hiyo
Mkutano huo wa kawaida wa Baraza kuu la Vijana wa CCM Mkoa wa Lindi pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa Nec Toka wilaya Nachingwea, Fadhil Liwaka pamoja na Mnec wa wilaya Hiyo Balozi Mchumo wakiwemo makatibu wa CCM wa Wilaya wakiongozwa Na Mwenyekiti wa CCM mkoa Mzee Ally Mohamed Mtopa