Ajali hii imehusisha gari aina ya Toyota yenye namba za usajili SU 39179 gari hii imetokea muda mfupi ulio pita katika eneo la soko kuu mjini lindi,
Dereva wa gari hilo alilitumbukiza gari hilo katika moja ya Shimo la Karavati lililokuwa katikati mwa barabara ni muda mrefu shimo hilo liko wazi bila ya kufanyiwa matengenezo yoyote Bado haijajulikana nani mwenye dhamana ya Kutengeneza barabara hii kama ni manispaa au ni Tanroad kwani kabla ya kuwepo kwa bara bara mpya inayotoka Dar es salaam kuelekea miji ya Mtwara Masasi Na Ruangwa Barabara hii ilikuwa inatumika kama Bara bara kuu.
Katika Ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa isipokuwa gari lenyewe tu ndio limeharibika.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.