AJALI MBAYA YATOKEA MKWAJUNI–LINDI

DSC_0213Mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Burhan Islam(fundi wa gari) amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Fuso
kugonga lori lingine nae kubanwa na bodi na kuokolewa baada ya
jitihada zilizofanywa na baadhi ya Abiria waliokuwa wakisafiri katika
barabara kuu ya Dar es salamu kwenda Mtwara na Lindi.
DSC_0127Gari hilo lenye namba za usajiri T 56ANQ lililokuwa likiendeshwa na
Kunja Mshamu limepata ajali hiyo leo katika kijiji cha Mkwajuni
wilayani Lindi baada ya kutaka kulipita gari lenye namba za usajili
T 402 AJG Scania lililokuwa likiendeshwa na Amos Chadenyile na
kushuhudiwa na BLOG HII jitihada zilizokuwa zinafanywa kuokoa
maisha ya kijana huo.
DSC_0221Majeruhi huyo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo alikimbizwa katika kituo cha afya kitomanga kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Uchunguzi zaidi
Katika ajali hiyo iliyousisha malori hayo hakuna majeruhi mwingine
aliepata jeraha huku gari hiyo ya Fuso likiwa limeharibika sanaDSC_0269

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post