Unknown Unknown Author
Title: SAMATTA,ULIMWENGU WAIPELEKA TP MAZEMBE NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wachezaji toka Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu hii leo (Jumamosi)waling’aa na kuisaidia klabu yao ya Tp Mazembe kufuzu hatua ya...

clip_image001Wachezaji toka Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu hii leo (Jumamosi)waling’aa na kuisaidia klabu yao ya Tp Mazembe kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho .

Wachezaji hao wa nafasi za ushambuliaji walikuwa nyota wa mchezo kati ya Tp Mazembe na Entente Sportive Setiff ya Algeria ambao klabu hiyo toka Congo 4-2 katika mchezo uliopigwa huko Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Football - 2012 CAF Champions League - Power Dynamos v TP Mazembe - Arthur Davies StadiumThomas Ulimwengu alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo huku moja likiwa linatokana na krosi ya Mbwana Samatta ambaye alifunga bao la nne la mchezo huo .

Bao lingine la Tp Mazembe lilifungwa na mkongwe na nyota wa timu hiyo Tressor Mabi Mputu huku Setif wakipata mabao yao kupitia kwa Mohamed Zeiti na Kaled Gourmi.IMG_9529Bao la Samatta linamfanya aongoze chati ya wafungaji kwenye michuano ya msimu huu ya kombe la shirikisho ambapo amefikisha mabao matano (5) akiwa na wastani wa kufunga kwenye karibu kila mechi kuanzia hatua ya makundi ilipoanza .

Matokeo haya yanamaanisha kuwa Tp Mazembe wamefuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho wakiwa wamejikusanyia pointi 10 baada ya michezo mitano huku wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja kabla ya hatua ya makundi kumalizika .

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top