Unknown Unknown Author
Title: DEREVA APOKEA KICHAPO KIKALI MARABAADA YA KUMGONGA DEREVA BODABODA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz video,Kilwa WAKAZI wa kijiji cha Kiranjeranje wilayani Kilwa Mkoani Lindi walifunga barabara kuu ya kibiti, Lindi Mtwara kwa k...

k (16)

Na Abdulaziz video,Kilwa
WAKAZI wa kijiji cha Kiranjeranje wilayani Kilwa Mkoani Lindi
walifunga barabara kuu ya kibiti, Lindi Mtwara kwa kuweka magogo, na mawe na kusababisha abiria na magari zaidi ya 50 kukaa kwa kipindi cha masaa kadhaa kabla ya kutawanywa na kikosi cha kutuliza Ghasia (
FFU).

Tukio hilo limetokea baada ya mwendesha bodaboda mkazi wa kijiji hicho Bakari Magoyo (38) kugongwa na gari namba T489 AGA wakati alipokuwa anavuka barabara hiyo.k (20)Wakizungumza kwa niaba ya wananchi Wenzao waliokuwepo baada ya kutawanywa kwenye tukio hilo, wakazi hao walisema kuwa wameamua kufunga barabara hiyo kwa kuweka mawe na magogo ili kuishinikiza serikali kuweka matuta ya kupunguza mwendo kasi wa magari kwenye eneo la makazi ya watu na ajali zinazofululiza katika eneo hilo.

Alipotakiwa kuongea globu Kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi badala yake wafuate kanuni na taratibu za kisheria ambapo Mwakajinga alieleza kusikitishwa kwake na tukio la kupigwa kwa Dereva wa gari hilo, Omary Mkuwili huku gari lake likivunjwavunjwa na kuibiwa karibu vifaa vyote baada ya ajali hiyo.

Aidha alibainisha kuwa Mwendesha pikipiki aliyegongwa alikimbizwa
hospitali ya mkoa ya Sokoine kwa ajili ya matibabu zaidi huku dereva
wa gari iliyogonga alipata majeraha makubwa baada ya kupata kipigo
na wananchi wenye hasira kali.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top