RUTO NA SANG WAKANA MASHTAKA ICC

clip_image002Kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague.

Bwana Ruto anayetuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, alikana mashtaka yote dhidi yake. Vile vile mshtakiwa mwenza mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang pia alikana mashtaka.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post