MAYWEATHER AMDUNDA VIBAYA SAUL ALVAREZ

clip_image002Alfajiri ya leo Bondia Mayweather amefanikiwa kumshinda Saul Alvarez wa Mexico ambaye kabla ya hapo alikuwa
hajapoteza pambano hata moja.Jaji wa kwanza alitoa sare ya pointi 114-114, lakini wawili wakatoa ushindi kwa Mayweather kwa pointi 116-112, 117-111.

Mayweather alitawala karibia raundi zote kuanzia ya tatu akipiga ngumi moja moja za kudokoa ambazo zilimzidi Mmexico huyo.

Kwa upande wa raundi, Mayweather alishinda kila raundi kuanzia ya kwanza hadi ya 12.Alvarez alionyesha uwezo kwa kupambana hadi mwisho, hata hivyo Mayweather alionyesha ni bora zaidi yake kiufundi.

Namna alivyokuwa anakwepa na kupiga, alimpa wakati mgumu Alvarez ambaye pia alionyesha atakuwa tishio zaidi.Still champion: Floyd Mayweather was hugely impressive in beating Saul Alvarez over 12 rounds in Las VegasHilo lilikuwa ni pambano la kwanza la Alvarez kupoteza baada ya kucheza mapambano zaidi ya 40, huku Mayweather akiendelea na rekodi ya kutopoteza.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post