Unknown Unknown Author
Title: MAAZIMISHO YA MTO MARA YAFUNGULIWA RASMI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Gabriel Tuppa akisalimiana na na baadhi ya viongozi na wazee wa mji mara tu baada ya kuwasili katika viwanja vya...

clip_image002Mkuu wa Mkoa wa Mara John Gabriel Tuppa akisalimiana na na baadhi ya viongozi na wazee wa mji mara tu baada ya kuwasili katika viwanja vya maazimisho.Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa akiwasalimia wananchi walio hudhuria maazimisho ya Mara day.Mkuu wa Mkoa wa Mara John Gabriel Tuppa akipewa maelezo juu matumizi shirikishi ya vyanzo vya maji katika banda la Wizara ya Maji.Mkurugenzi Masidizi Rasilimali za Maji Wizara ya Maji, Mhandisi Dk. George Lugomela akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa namna ya matumizi ya pamoja ya maji kutoka kwenye vyanzo vya maji.Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mkurugenzi Masidizi wa Rasilimali za Maji Wizara ya Maji, Mhandisi Dk. George Lugomela wakipokea maelezo namna Wizara ya maji inavyokabiliana na magugumaji katika maziwa na mito nchini. Picha na Athumani Shariff, Wizara ya Maji

Na Athumani Shariff, Wizara ya Maji

Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa ameyafungua rasmi maazimisho ya siku ya mto Mara katika viwanja vya Jamhuri Mugumu Wilayani Serengeti Mkoa wa Mara.

Hii ni mara ya kwanza kwa maazimisho hayo kufanyika nchini Tanzania na ni mara ya pili tangu kuanzishwa kwake baada ya makubaliano yaliyofanyika Kigali, Rwanda,  baina ya viongozi wakuu wanchi za maziwa makuu Aprili mwaka 2012 na kufanyika Kenya Septemba 15 mwaka jana kwa mara ya kwanza.

Maazimisho hayo yenye kaulimbiu “Mara ni mali yetu na urithi wetu tuitunze” yana lengo la kuulinda na kuutunza mto Mara ambao chanzo chake ni mlima Mau uliopo nchini Kenye na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria ambalo linaunganisha nchi za Tanzania, Kenya pamoja na Uganda.

Mkuu wa Mkoa wa Mara amewataka wakazi wote wananokaa karibu na mto Mara wautunze na kuulinda mto huo kwa kutofanya uharibifu wa aina yoyote kwani ni muhimu sana.

“Wananchi tuutunze mto ule, tuulinde mto ule, anayepaswa kutunza ni sisi. Mto huu unamanufaa kwa binadamu, wanyama mazingira na viumbe vyote.

Sote tuongee lugha moja ya kuutunza mto huu, tusilime kando ya mto, wala tusifuge na kunywishia wanyama pembezoni mwa mto wetu”. Alisema Mkuu wa Mkoa. Pia aliwataka wananchi kutumia fursa hii ya maazimisho kujipatia elimu juu ya umuhimu wa utunzaji wa mto huu.

“Hebu jifunzeni, mupate manufa ya maonesho haya. Tupite kwenye mabanda haya na tujifunze namna mbalimbali za utunzaji mto wetu.” Alisisitiza Mheshimiwa Tuppa.

Kadhalika aliwasisitiza wakazi wa Serengeti kuwa wakarimu kwa wageni wote kutoka nchi zote. Alisema wawasaidie wageni pindi watakapo hitaji msaada.

Alisisitiza kuwa Mara ya leo tofauti na ile ya zamani ya vurugu, ugomvi na uadui. Kilele cha maaazimisho haya itakuwa ni tarehe 15 Septemba kama ilivyoamuliwa na nchi wananchama, na mgeni rasmi anategemewa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Maazimisho ya mto Mara maarufu kama Mara Day yatakuwa yakifanyika kwa kupokelezana baina ya nchi za Tanzania na Kenya ambao ndiyo wadau wakuu wa mto huo. Mto Mara ni kivutio kikubwa kutokana na kitendo cha kuvuka kwa nyumbu kutoka Serengeti Tanzania na kwenda Masai Mara Kenya, kitendo ambacho hujirudia na kugeuka kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top