Unknown Unknown Author
Title: CRDB BANK YAZIDI KUFUNGUA FURSA KATI YA TANZANIA NA CHINA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wakisoma vipeperushi vyenye taarifa za huduma mbalimbali za benki hiyo wakati wa maonesho ya bidhaa za Chi...

clip_image001Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wakisoma vipeperushi vyenye taarifa za huduma mbalimbali za benki hiyo wakati wa maonesho ya bidhaa za China yanayofanyika Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa benki hiyo anayesimamia Dawati la China, Ibrahim MasahiMeneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Kitengo cha Dawati la China, Ibrahim Masahi akitoa ufafanuzi kuhusu huduma wanazotoka kwa raia wa China wakati wa maonesho ya bidhaa za China.Watu mbalimbali waliojitokeza katika maonesho hayo wakipata maelezo huduma za kibenki katika banda la benki ya CRDB.Ofisa Masoko wa benki ya CRDB, Gerald Mhalanyambu (kulia), akitoa maelezo ya huduma wanazotoa kwa baadhi ya watu waliotembelea banda lao.Wateja wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na benki ya CRDB.Maofisa wa benki ya CRDB, Ibrahim Kasahi (kushoto), Ninael Munuo na Gerald Mhalanyabu.

DAR ES SALAAM, Tanzania

HUDUMA ya Dawati la China katika Benki ya CRDB imepata mafanikio makubwa kwa kuchangamkiwa na wateja wengi tangu ilipozinduliwa rasmi Machi 27, mwaka huu. Kuwasaidia wafanyabiashara wa Tanzania wanokwenda China

Akizungumza katika banda la CRDB kwenye Maonyesho ya Biashara ya China, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, jana, Meneja Mahusiano anayesimamia dawati la China, Ibrahim Masahi alisema, zaidi ya fedha za China Yuan milioni 55 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 14.3 zimeweza kubadilishwa kupitia huduma ya dawati hilo.

Masahi alisema, tangu huduma hiyo izinduliwe CRDB imepata ongezeko la asilimia 70 ya wateja, wanaotumia hudum hiyo ambao ni Watanzania wanaokwenda China au Wachina wanaokuja Tanzania kwa ajili ya shughuli za biashara au matembezi.

Alisema, kupitia dawati hilo, kuna kuna huduma ya UnionPay ambayo ni sawa na Master Card au Visa Card zinazomwezesha mteja kutoka Tanzania kuchukua fedha kwenye ITM ya benki yoyote akiwa nchini China, kadhalika inamwezesha pia anayetoka China kuchukua fedha kwenye ITM za CRDB akiwa Tanzania.

Masahi alisema, ili kuboresha huduma hiyo ya Dawati la China, CRDB imeweka mahusiano ya kibishara na Benki mbili nchini China ambazo ni Bank Of China HBC ya Beijing nchini humo kwa ajili ya huduma ya kusafirisha fedha kiwa haraka zaidi kutoka Tanzania kwenda huko.

“Kama siyo tofauti ya muda kati ya Tanzania na China, wateja wetu wangekuwa wanapata fedha ndani ya saa 24, hata hivyo haiichukui muda mrefu mtenja aliyeko China kupata fedha tunayomtumia kutoka hapa Tanzania”, alisema Masahi.

Maonyesho hayo ya aina yake, ambayo yalifunguliwa jana, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, yanashirikisha kampuni zaidi ya 100 kutoka China ambazo zinaonyesha bidhaa mbalimbali zikiwemo za nyumbani na za kiteknolojia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top