Unknown Unknown Author
Title: BG TANZANIA KUIMARISHA USALAMA BARABARANI MKOANI LINDI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mhandisi Dk. Ezekial Mganilwa, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (aliyesimama ) anamualika mgeni rasmi Mheshimiwa Saidi Mtanda, Mbunge...

clip_image001Mhandisi Dk. Ezekial Mganilwa, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (aliyesimama ) anamualika mgeni rasmi Mheshimiwa Saidi Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga (aliyevaa shati nyeupe).Mheshimiwa Saidi Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga akizindua mafunzo ya uendeshaji Piki Piki huku akimpa mkono Mkuu wa masuala ya Sera na Ushirika wa kampuni ya BG Tanzania, Fred KiboyaMhandisi Dk. Ezekial Mganilwa, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji akimpa mkono Mkuu wa masuala ya Sera na Ushirika wa kampuni ya BG Tanzania, Fred Kiboya.

Leo tunashuhudia uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani unaofadhiliwa na BG Tanzania katika mkoa wa Lindi, kusini mwa Tanzania. Baada ya kupewa kazi ya kufanya utafiti kuhusu ajali za barabarani na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kampuni ya gesi ilibaini fursa za kushirikiana katika kuimarisha maadili ya usalama barabarani miongoni mwa wakazi wa Lindi .

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kilibaini visababishi vinne vya mara kwa mara vya ajali za barabani mkoani Lindi ambavyo ni: waendesha pikipiki wasiozingatia maadili ya uendeshaji; mwendo kasi wa waendesha pikipiki;kuendesha huku umelewa; na ukosefu wa alama au ishara za barabarani. BG Tanzania imeazimia kupunguza kiwango cha ajali kwa kufadhili utoaji wa mafunzo ya usalama barabarani. Hii inaenda sambamba na juhudi za mkoa katika kupunguza ajali za barabarani.

Mkuu wa masuala ya Sera na Ushirika wa kampuni ya BG Tanzania, Fred Kiboya, alihudhuria kwenye sherehe na alisema

“Hili ni tukio muhimu kwa BG Tanzania. Kama kampuni tunaamini katika usalama, na tunataka kuhakikisha kuwa, uwepo wetu kusini mwa Tanzania unajenga jamii salama na zenye mafanikio zaidi.Tunaendesha programu ya aina hii Mtwara Mjini, ambapo waendesha pikipiki 600 wanapatiwa mafunzo, na sasa tunarudia zoezi mkoani Lindi.”

Mkoani Lindi, waendesha pikipiki mia mbili watanufaika katika awamu ya kwanza ya programu hii. Kila mmoja atapewa mafunzo ya zaidi ya siku kumi ambapo siku sita zitakuwa kwa ajili ya mafunzo ya nadharia na siku nne zitakuwa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Hii itajumuisha utambuzi wa alama na ishara za barabarani, nadharia za uendeshaji wa kujihami,uendeshaji unaofaa, mkao sahihi katika uendeshaji na udhibiti.

Baada ya kumaliza mafunzo kwa ukamilifu, washiriki watapewa cheti cha umahiri katika uelewa wa usalama barabarani pamoja na leseni ya uendeshaji. Kundi la washiriki limechukuliwa kutoka katika kata za mchinga, Kitomanga, Rutamba, Nyangao na Milola.

Gharama za mafunzo ni Sh. 220,000/-kwa kila mshiriki, hii ikimaanisha kwamba, kwa ujumla, BG Tanzania imewekeza Shilingi 44,000,000/- kwa ajili ya mafunzo na upatikanaji wa leseni katika awamu hii. Awamu ya pili,ambayo itajumuisha waendesha pikipiki wengine 200 itapangwa baadaye.

Mgeni rasmi kwenye tukio alikuwa Mheshimiwa Saidi Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga; ambapo Mhandisi Dk. Ezekial Mganilwa, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji aliiwakilisha taasisi yake. Bwana Machumu Leonard, Afisa wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Lindi alihudhuria akiiwakilisha Ofisi ya Kamishina wa Polisi wa Mkoa pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ACP Mwakanjiga

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top