BAADA YA KUANGUKA JUKWAANI HII NDO KAULI YA LADY JAY DEE

clip_image001Kama uliangalia Diary of Lady Jaydee wiki iliyopita, ulimshuhudia staa huyo akifanya shopping ya viatu kwaajili ya show yake ya Kili Music Tour jijini Dar es Salaam weekend iliyopita.

Lady Jaydee akiwa backstage na kiatu chake kilichosabisha ateleze jukwaani Katika show hiyo Lady Jaydee alinunua kiatu cha rangi ya blue, kirefu aka high heels chenye thamani ya shilingi 168,000. Yes laki moja na elfu sitini na nane kama masikio yetu hayakutudanganya.

Hata hivyo urefu wa kiatu hicho ameutaja kuwa chanzo cha kuteleteza jukwaani kwenye show hiyo na kukaribia kumwangusha.
“Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali zingine, isitoshe sikuanguka bali nilikaribia. Ila poleni kwa mlioumizwa na hicho kitendo…Nitapunguza urefu wa viatu siku nyingine,” aliandika jana kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Ni bahati mbaya tu, kwani hata Mwanza/Kahama/Dodoma vilikuwa virefu kama hivyo hivyo na sikuteguka,” alitweet kufafanua kuhusu uvaaji wa viatu virefu jukwaani.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post