ANGALIA KILICHOJIRI KATIKA MSIBA WA MSANII WA FILAMU

clip_image001Mama mzazi wa Malisa akiwa na uso wa huzuni.

VILIO vimetanda msibani kwa msanii wa filamu za Kibongo, Zuhura Maftah ‘Malisa’ aliyefariki dunia jana akiwa hospitali ya Hindu Manndal alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.
Msiba wa msanii huyo upo nyumbani kwa dada yake Mikocheni na mazishi yatafanyika kesho makaburi ya Kinondoni.
Dada wa marehemu (wa tatu kushoto) akilia kwa uchungu baada ya msanii wa filamu, Chuchu Hansi (aliyeinamisha kichwa) kuingia na kuangua kilio.Wasanii wakongwe wa filamu, Devotha Mbaga na Vanitha wakilia kwa uchungu.Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.

(Habari/Picha: Gladness Mallya na Hamida Hassan / GPL)

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post