CESC FEBREGAS AMTABIRIA MAZURI OZIL

clip_image001Nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas amemtabiria mchezaji mpya wa Gunners, Mesut Ozil kutikisa katika Ligi Kuu ya England.

Fabregas aliondoka klabu hiyo Kaskazini mwa London kuhamia Barcelona mwaka 2011, lakini bado ana ukaribu klabu hiyo.

Anaamini mchezaji huyo nyota wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 atang'ara katika Ligi Kuu ya England.

Akizungumza na Al Primer Toque, Fabregas alisema: "Anakwenda kufurahia katika Ligi Kuu England tena sana tu. Ni ligi yenye nafasi zaidi na Ozil ni mchezaji wa aina hiyo, ukimpa muda na nafasi, anakuua.

Kama ambavyo tumeona wakati akiwa Real Madrid, mpira wake wa mwisho ni hatari na naamini kwamba atafurahia England,"amesema. Ozil anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza The Gunners dhidi ya Sunderland Uwanja wa Light Jumamosi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post