Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akifunga bao la kuongoza
KOCHA Arsene Wenger ameanza vibaya Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Aston Villa Uwanja wa Emirates leo.
Kocha huyo Mfaransa amesaini mchezaji mmoja tu ambaye pia ni majeruhi baada ya kutemwa wachezaji 17.
Wachezaji wawili wa Arsenal, Keiron Gibbs na Alex Oxlade-Chamberlain walilazimika kutoka nje kipindi cha kwanza baada ya kuumia na Christian Benteke alikuwa kinara wa ushindi wa Villa.
Benteke alifunga mabao mawili katika dakika za 21na 60 wakati bao lingine lilifungwa na Luna dakika ya 84, wakati Arsenal ilitangulia kupata bao dakika ya tano kupitia kwa Olivier Girous.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna/Podolski dk90, Koscielny, Mertesacker, Gibbs/Jenkinson dk5, Wilshere, Ramsey, Rosicky, Walcott, Chamberlain/Cazorla dk5 na Giroud
Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker/Clark dk7, Luna, El Hamadi, Westwood, Delph, Agbonlahor, Weimann/Bacuna dk88 na Benteke,
Takwimu za mechi ya Arsenal na Aston Villa
Giroud akishangiliaAmeokoa: Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny akipangua mkwaju wa penalti wa Benteke......lakini Benteke akafunga baada ya kuuwahi mpira uliorudiDamu: Mchezaji wa Arsenal, Kieran Gibbs akiigulia maumivu chini baada ya kugongana na Andreas Weimann wa VillaGibbs akitolewa baada ya kuumia kichwaMchezaji wa Villa, Ron Vlaar, wa pili kulia akiokoaMchezaji wa Arsenal, Tomas Rosicky, chini akipambana na Karim El Ahmadi wa VillaUtata: Santi Cazorla, Per Mertesacker na Wojciech Szczesny wakiwa hawaamini refa Anthony Taylor amewapa Villa penalti ya piliShabiki wa Arsenal akipeleka wa wazi kwa Wenger kumtaka asajiliMwanzo mbaya: Wenger akisikitika baada ya kipigo
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.