MABINGWA wa England, Manchester United, leo wameanza kampeni yao ya kutetea Taji lao Ugenini huko Liberty Stadium kwa kuinyuka Swansea City Bao 4-1.
Wakiwa chini ya Meneja mpya, David Moyes, alietwaa wadhifa huo baada ya kustaafu kwa Lejendari Sir Alex Ferguson, Man United walianza Mechi hii kwa kuidhibiti vizuri Swansea City ambayo ilimiliki vizuri mpira na kutawala katikati.Kazi njema ya Mkongwe Ryan Giggs ndio iliyofungua milango ya Magoli kwa Robin van Persie kufunga Bao zuri la kifundi na Dakika mbili baadae Valencia alimtengenezea vyema Danny Welbeck aliemalizia kirahisi na kuandika Bao la pili. Hadi Mapumziko, Swansea 0 Man United 2.Straika Wayne Rooney, aliekumbwa na majeruhi na kugubikwa na madai ya kutaka kuhama, aliingizwa katika Dakika ya 62 na muda mfupi baadae Robin van Persie alifunga Bao lake la Pili kwa shuti kali.
Katika Dakika ya 82, dhihaka za Welbeck zilizaa Bao kwa Swansea alipopokonywa mpira na kupasiwa Mchezaji mpya wa Swansea anaetoka Ivory Coast, Wilfried Bony, alieipatia Swansea Bao lao pekee.
Rooney ndie aliesababisha Bao la 4 kwa kumpa pande safi Danny Welbeck aliemvalisha kanzu Kipa Vorm na kufunga Bao la 4.
Mechi inayofuata ya Ligi ya Man United ni huko Nyumbani kwao Old Trafford hapo Jumatatu Agosti 26 dhidi ya Chelsea.
VIKOSI:
Swansea: Vorm; Rangel, Flores, Williams, Davies; Dyer, Britton, Canas, Shelvey, Routlege; Michu
Akiba: Tremmel, Amat, Taylor, Kit, Pozuelo, Hernandez, Bony
Man United: De Gea; Jones, Ferdinand, Vidic, Evra; Valencia, Carrick, Cleverley, Giggs; Welbeck, van Persie
Akiba: Lindegaard, Fabio, Smalling, Anderson, Zaha, Kagawa, Rooney.
LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumamosi 17 Agosti
Liverpool 1 Stoke City 0
Arsenal 1 Aston Villa 3
Norwich City 2 Everton 2
Sunderland 0 Fulham 1
West Bromwich Albion 0 Southampton 1
West Ham United 2 Cardiff City 0
Swansea City 1 Manchester United 2
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.