Suarez alikuwepo kwenye kikosi cha Uruguay leo kilichoifunga Japan 4-2
MSHAMBULIAJI aliye katika wakati mgumu, Luis Suarez amekanusha taarirfa kwamba leo alisema yuko tayari kurudi kazini na kubaki Liverpool.
Mchezaji huyo anayetakiwa na Arsenal amenukuliwa katika mahojiano kutoka nchini Japan na gazeti la Uruguay, El Observador akisema angebaki Anfield kwa sababu ya jinsi aanvyoungwa mkono na mashabiki wa Liverpool.
Lakini akizungumza baada ya kuiwezesha Uruguay kuifunga Japan 4-2 katika mchezo wa kirafiki, Suarez alikanusha na kusema hajabadilisha moyo wake.
"Sikusema hivyo, labda mtu mwingine alifanya hivyo na kitu cha msingi ni kwamba, nipo hapa kwa sasa na timu ya taifa," Shirika la Habari la Japan, Kyodo limenukuu akisema.
Suarez (kushoto) akishangilia na mshambuliaji pacha wake, Diego Forlan baada ya kuifungia bao la tatu UruguayKatika mpambano kamili: Suarez alidaiwa kusema upendo wa mashabiki unamfanya abaki, kabla ya kukanusha taarifa hizo
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.