Unknown Unknown Author
Title: KUMBE WENGINE BARABARANI NI FEKI, TRAFFIC FEKI ANASWA DAR ES SALAAM AKIWA KAZINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Huyu ndiye Traffic feki baada ya kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Stakishari Dar es Salaam,Tanzania MTU mmoja ambaye ji...

clip_image001Huyu ndiye Traffic feki baada ya kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Stakishari

Dar es Salaam,Tanzania

MTU mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikamatwa jijini Dar es Salaam, baada ya kuvaa sare za Jeshi la Polisi wa Usama Barabara (Traffic) nchini Tanzania akiwa Barabarani akiendelea kutekeleza jukumu la Jeshi hilo.

Askari wa Polisi wa Usalama wa raia,Barabarani na Magereza huajiriwa chini ya sheria za utumishi wa Umma zinazosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.Askari huyo bandia alikamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare.

Tanzania kama zilivyo nchi zingine zote duniani, zinatekeleza sheria za Barabarani kwa Askari kuwa Barabarani muda wote kwa lengo la kuangalia Uslama wa Brabarani kwa watumiaji wa aina zote.

Hata hivyo nchini Tanzania kazi hiyo imekuwa ikipokelewa kwa hisia tofauti kiasi cha kushawishi baadhi ya raia kuwania nafasi ya kuwa Asakari wa Usalama Barabarani ama kudanganya kuwa Askari kama ilivyotokea kwa Askari huyo feki.

clip_image001[7]Traffic feki akiwa katika gari la Polisi akipelekwa katika kituo cha polisi baada ya kukamatwa.

Moja ya sababu ya matukio hayo ni kitendo cha Askari wa Uslama Barabarani kularushwa nyingi, kwa kuwakamata madereva na kuwalazimisha kutoa rushwa kutokana na makosa yao ama makosa ya vyombo vya vya usafi na wakati mwingine askari hao huwasingizia madereva hao kuwa na makosa katika mazingira ambayo si halisia.

Hata hivyo askari huyo feki alipelekwa katika Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake, akiwa na sare zake pamoja faili ambalo hutumiwa na askari hao.

SOURCE: HABARI MPYA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top