Sehemu: 10
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633
Ilipoishia…
“Adela”
…Mikononi mwao kila mmoja alionesha kushikilia mienge iliokuwa ikitoa moto mkali kuangaza. Wakawa wakinisogelea karibu zaidi. Wakajitokeza Sonia na Sarah wakiwa wameshikilia mioyo mingi zaidi ya ile niliokuwa nimeitupa. Wakanirushia ile mioyo hadi ndani ya tope. Wale mbung’o waliokuwa wakinishambulia wakaiwahi ile mioyo nakuiteketeza. Ikanyumbulika! Halmashauri ya kichwa changu ikafanya kazi haraka nakujua huenda mimi leo ndo kitoweo chao...
Songa nayo…
“Adela! Adela!”
Waliita kwa pamoja Sonia na Sarah. Sauti zao ziliendelea kuita uku zikijirudia midomoni mwao mara mbili mbili. Wale wachawi wao walikuwa bado wakishikilia mienge iliokuwa ikitoa moto uku wakiinua kwa juu. Walikuwa wamepoza sauti zao kupisha sauti za Sonia na Sarah. Sonia na Sarah ambao bado walikuwa wamebakiwa na mioyo miwili miwili kila mmoja mikononi mwao. Wakanirushia tena kwa mara ya pili.Wale wachawi wakaanza upya kuimba ile nyimbo niliokuwa nikiipenda.Wakashangilia!
“Adela unatakiwa kuila hiyo mioyo yote haraka iwezekanavyo!”
Aliongea Sonia kwa sauti ya juu. Kitendo cha kuongea tu wale mbung’o wakaiwahi tena ile mioyo iliyokuwa imerushwa na Sarah na Sonia. Wakaifakamia na kufurahia kupata kitoweo pasipo jasho. Nikainua mikono yangu nakuanza kunyang’anyana na mbung’o wenye njaa kali.Mbung’o wakatawanyika nakuniachia ile mioyo.Wakakimbilia maeneo ya kifuani mwangu kama walivyokuwa wakifanya awali. Wakazidisha kutengeneza duara kubwa katika maeneo niliokuwa nimekatwa matiti. Maumivu makali yakaanza kupenya katika mwili wangu. Nilijikuta nikiambulia kushika moyo mmoja tu uku ile mingine nikiiachia. Nikaushikilia kwa nguvu na kwa hisia zote. Nikaufinya ule moyo katika kiganja changu mpaka ukawa laini sana mithili ya maini. Nikausogeza mpaka maeneo ya mdomoni mwangu nakuutafuna. Kadri nilivyokuwa nikiutafuna ndivyo na mapafu yangu mwilini yalivyokuwa yakinitanuka. Yakazidi kutanuka nakusababisha tumbo lionekane kubwa sana. Mpasuko! Mwili wangu wote ukasambaratika kuanzia mikono tumbo mpaka kiuno na miguu vikasambaa. Adela mimi nikabakiwa kichwa peke yake uku nusu ya mwili wangu ukiwa umesambaratika juu ya tope.. Mdomo ukawa hauna tena uwezo wa kutoa sauti na kuongea zaidi ya macho yangu kuangaza mbele. Mbele kulipokuwa kumezungukwa na idadi ya kundi kubwa la wachawi wakiwa wameshikilia mienge inayowaka moto wakiongozawa na Sarah na Sonia.Akili ikaumia sana kuukosa moyo.Moyo uliokuwa ukimsaidia kwa mawazo. Moyo ambao tayari ulikuwa umeshajikusanya na viwili wili kusambaratika juu ya tope.Mchawi yeyote anaweza hata kukatwa kichwa na bado akawa anaongea kama waongeavyo binadamu wa duniani. Hiyo ni nguvu ya ajabu waliokuwa nayo wachawi wote.
**************
“Adela?”
Sauti ya Sophy ikashtua ngome ya masikio yangu.Macho yangu bado yalikuwa yamefumba japo masikio yalikuwa wazi kusikia chochote. Nikatoa macho kuangaza Sophy alipo.Ubaridi mkali bado uliendelea kutawala katika shingo yangu iliokuwa imeachanishwa na kiwili wili. Lile eneo niliokuwa nimelalia tope uku mbung’o wakinitafuna halikuwepo tena mbele ya macho yangu. Kichwa changu kikawa kama kimehifadhiwa chini ya mti mkubwa. Kichwa tupu! Sikuweza kujigeuza nakutambua sauti ya Sophy ilipokuwa ikitokea.
“Adela jamani! Pole sana Adela!”
Sauti ya Sophy ikawa bado ikiniongelesha uku hisia za kuwa yupo maeneo ya karibu nikiwa nazo. Tahamaki! Macho yangu yakakutana uso kwa uso na Sophy. Sophy aliyekuwa mtupu kama alivyozaliwa. Akanishika kichwa changu nakukiweka kwapani.
“Twende!”
Alionesha kuwa na hasira kali kwani hata macho yake hayakuwa ya kawaida. Alinishikilia kwa nguvu kwapani mwake. Shingo yangu ndio kwanza ilizidiwa na baridi kali hali ilionifanya nisikie upepo mkali ukinitoka kupitia puani, masikioni na mdomoni. Upepo mkali uliojawa na vumbi. Sikuweza kupiga hata chafya japo hisia za kupiga chafya nilikuwa nazo. Nikatamani sana nimuulize Sophy tunapoelekea lakini hali ikawa pale pale kwamba sikuwa na uwezo wa kutoa sauti zaidi ya kusikia tu. Baada ya Sophy kutembea kwa umbali kidogo masikio yangu yakaanza tena kusikia ile nyimbo niliokuwa nikiipenda ikiimbwa na wachawi kwa mbali. Ile sauti ya nyimbo ikaonekana kumkera sana Sophy. Akachukua kichwa changu nakukiweka mbele ya uso wake. Akatikisa kichwa chake kwa hasira kali alizokuwa nazo. Ule uso wake ukabadilika rangi nakuwa na sura ya yule mmama aliyenileta uku kwenye himaya hii ya wachawi wengine. Sura ya Sophy ikabadilika tena ikawa kama ya Sonia mara kama ya Sarah. Akachukua kichwa changu nakukitupa mpaka chini. Nikahisi kama napasuka kichwa. Kichwa changu kilibiringita zaidi ya mara ishirini mithili ya mpira wa miguu kisha kikagota karibia na mti mkubwa. Nikaanza kuvuja damu si damu kwani ilikuwa ni ya bluu sana. Ikaanza kunitoka kuanzia masikioni. Masikio yote mawili yakatoa damu damu za bluu mithili ya bomba litoavyo maji kwa wingi.Masikio yakashirikiana na pua katika kutoa damu damu nakupelekea mdomo kushikwa tamaa ya kutoa damu. Mdomo nao ukaanza kufurahia kutoa damu damu.Nikaachama uku nikitoa ulimi nje nakuruhusu damu damu zile zinitoke kwa nguvu zote. Nikayatoa macho ya ukali kumuangalia yule niliyedhania ni Sophy mbele yangu. Nikashuhudia akisinyaa nakuwa mdogo sana kama panya. Akakimbia!
Zile damu damu zikaanza kujikusanya nakuweka mstari mmoja. Zikatawanyika kwa kufuata mkondo mmoja uku zikitokomea ndani ya pori zaidi. Zikakata kutoka katika sehemu zangu za masikioni,puani na mdomoni. Macho yakaanza kuangaza sehemu damu zilipokuwa zikielekea. Misukule watatu wakatokea katika ile sehemu damu ilipotokomea. Walikuwa wamebebeshana mwili wa mtu alioonekana mwanamke kutokana na kuwa na matiti kifuani mwake uku akiwa hana kichwa zaidi ya kubakiwa na shingo pekee. Wakasogea mpaka karibu na kichwa changu kilipo. Wakaangusha ule mwili wa yule mtu. Wakajipanga mstari kuashiria kuna mtu anatokea katikati yao.
“Adela!”
Sauti ya Sonia sasa ikawa imeshakaririshwa rasmi na masikio yangu. Akatokea Sonia miongoni mwao.akainama mpaka chini nakushika kichwa changu. Akatoa tabasamu pana.Akanong’ona!
“Bado tunakupenda!”
Akanena kwa sauti ya kimya kimya masikioni mwangu. Masikio yakatingishika mithili ya mbuzi ‘beberu’ akitaka kufanya mapenzi na mbuzi jike.Akatoa ile dawa yetu ya wachawi ya “CHAYA” inayoweza kuunga kiungo chochote cha mchawi kikiharibika ama kukatwa. Sonia akaanza kunipaka nayo shingoni mwangu uku akisugua kwa nguvu zote.Alipomaliza alionesha ishara kwa ile misukule. Misukule ikainua ule mwili wa mwanamke uliokuwa chini. Sonia akatoa tena chaya nyingine nakupakla shingo ya ule mwili nakusugua kwa nguvu zote. Kisha akachukua kichwa changu nakukiunga na ule mwili. Vikang’ang’ana!
“Adela? Adela? Ongea basi?”
“Abee! Unasemaje?”
Nillijikuta naweza kutoa sauti, tena sauti tofauti na sauti yangu ya kawaida. Ilikuwa ni mchanganyiko wa sauti ya kike na ya kiume. Sauti iliyoshiba na yenye kumtetemesha mtu yeyote.Akili ikafurahia nakuanza kuutafuta moyo ndani yake ulipo.ukafanikiwa kuuona moyo nakufurahia kuwepo pamoja kwa mara nyingine.
******************
***** Adela amekuwa mchawi mpya tena katika himaya nyingine ya kichawi. Amekuwa na matiti. Vipi Sonia atamfanyaje baada ya hapo? Nini hatma ya Adela katika uchawi wake?
*** Vipi kuhusu kumalizia kulala na maiti ishirini? Ataendelea nazo? Nini hatma ya Adela?
**** Inamaana Chaya inaweza kumuunga mchawi yeyote. Dawa hii inatokana na mizizi ya mti wa mbuyu ambayo husagwa na kuwa unga unga.Unga wake unaponyesha mtu ambaye amejereuliwa. Kwa mujibu wa Adela.
**** Simulizi hii ni ya kweli na mambo yaliopo ni ya kweli kwa wachawi hakuna hata kimoja kilichobuniwa. Najua lazima kuna baadhi ya wachawi watakuwa wameiona simulizi hii ama kuambiwa na watu. Ni kwamba Adela ameahidi kuwaumbua wachawi wote na njia zao zinazotumika ili watu wa duniani wajue. Kwa pamoja tunaupinga uchawi.
***** LIKE nyingi zinasaidia kuifanya simulizi hii inoge na kuwa tamu zaidi. Gonga LIKE yako simulizi hii.
Tags
HADITHI NA RIWAYA