Story: Nililala na maiti 20 ili niolewe na Rais - 07
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633
Ilipoishia jana…
..Wakaanza kumtoboa Baraka mwilini mwake. Wakamtoboa kila kona ya mwili wake. Damu nyingi zikamtoka Baraka kupitia sehemu alizotobolewa. Wale mabinti wakakinga zile damu kila zilipokuwa zikitomka Baraka. kila mmoja akajaza damu katika bakuli lake. Baraka alilia sana.Akawa mwembamba sana kwa kukauka damu. Hakuwa na nguvu ya kuinuka wala kufanya chochote kutokana na kuwa tayari katika himaya ya kichawi. akapoteza fahamu kabisa.
“Adela? Shika kisu hiki?”
Baba Jamila akanikabidhi fupa kubwa lenye makali ambalo huliita kisu. Akanishikisha.Hofu ikanitanda!
“Adela? Unatakiwa umtoe utumbo wake wote nje halafu utaanza kuula wewe na kisha utanipa mimi na wageni wetu hapa utamkatia kila mmoja. Sawa?”
Songa nayo sasa…
Nikaendelea kulishikilia fupa lile vizuri huku macho yakinitoka vilivyo. Nikasogea hadi karibu na mwili wa Baraka. Baraka ambaye kwa sasa hakuwa akiweza kuona chochote zaidi ya macho yake kuyafumba. Hakuwa na kumbukumbu tena wala ufahamu.Wale mabinti wakatawanyika kila mmoja na bakuli lake lililojaa damu za Baraka. Nikiwa bado katika hali ya uchi wa mnyama huku eneo la matiti yangu yakiwa hayapo kutokana na maisha ya kichawi yanavyotaka. Nikatumia lile panga niliopewa na mzee taratibu nakuanza kumchana Baraka kifuani mithili ya ngozi ya mnyama ikichunwa. Muda wote wachawi wenzangu pamoja na wachawi waalikwa walikuwa pembeni yangu wakinizunguka. Walikuwa wakitazamana wenyewe kwa wenyewe wakinena kwa lugha za kichawi. Kadri zile nyimbo zilivyokuwa zikiimbwa ndivyo na mwili wangu ulivyokuwa ukiongezeka hisia za kichawi. Nikamchana Baraka tumboni mwake ishara ya duara kisha nikatoa ngozi ya juu nakushuudia utumbo wa Baraka ukiwa wazi.
“Oiyeee!! Oiyeee Adela!”
Aliropoka baba Jamila. Alikuwa akisifu kitendo cha mimi kufanikiwa kuutoboa mwili wa Baraka.Ujasiri! Nikalitupa lile fupa pembeni. Nikatumia mikono yangu miwili kuingiza mpaka tumboni mwa Baraka.Niliitumbukiza mpaka nikahakikisha ikikaribiana na mbavu za mgongoni mwake. Nikavuta nakutoka na rundo la utumbo utumbo. Nikauchukuwa mkono wangu mmoja nakuchukua lile fupa kama kisu. Mkono mwingine nikashikilia rundo la utumbo uliokuwa umechanganyikana na vitu kama mafuta mafuta nilivyokuwa nimevitoa tumboni mwa Baraka. nakainuka navyo mpaka juu. Nikatoa sauti ya ukali ya kichawi.
“Oiyeee!!! Baba Jamila Oiyeee!!! Ineku oiyee!!”
Kwa kawaida ya wachawi neno ‘Ineku” huwa linamaanisha wachawi waalikwa ambako kwa duniani huwa wanawaita wageni. Ineku wote wakainua mikono juu wakinishangilia kwa kuwa shujaa.Munkari!Nikaanza kuchabanga chabanga ule utumbo mpaka ukawa vipande vipande mithili ya wadudu wadogo dogo watambaao waitwao minyoo. Nikachukuwa kidogo nakuula huku damu damu zilizochanganyikana na mafuta meupe meupe ya ule utumbo yakinichuruzika pembeni ya mdomo wangu. Nikainama kwa mara nyingine nakuchukuwa vipande vya utumboi na kumpatia baba Jamila. Nikarudi tena mpaka chini nakubebelea rundo la nyama za utumbo nakuanza kusambaza kwa ineku wote. Nikawazunguka huku nikiwapa katika viganja vyao vya mikono. Wakajilamba! Kila nilivvokuwa nikiwapa ndivyo na mwili wangu ulivyokuwa ukijisikia nguvu za ajabu zilizoambatana na hisia za kichawi. Hatimaye nikamaliza kuwagaia wote wakaanza kufakamia ule utumbo niliokuwa nimeutoa tumboni mwa Baraka huku wakiimba nyimbo za kichawi kushukuru.
“Adela shika na hii?”
Baba Jamila aliniletea kitu kama msumeno chenye makali nakunikabidhi.
“Hiyo unatakiwa ukate kidole kimoja baada ya kingine uweke pembeni hapo. Hii hutusaidia kwenye kuruka na ungo kwani huwa inahifadhiwa ndani ya ungo.”
Bila kupoteza muda nikauchukuwa mkono mmoja wa Baraka nakuanza kumkata kidole kimoja baada ya kingine. Nikahamia mkono mwingine nao nikamkata vidole vyote nakuviweka pembeni yangu. Nilipomaliza mikononi nikahamia miguuni. Nikamkata vidole vya miguuni nakuviweka pembeni. Ndani ya dakika chache nikawa nimeshamaliza kumkata Baraka vidole vyote vya miguuni na mikononi. Nikavikusanya nakumpa baba Jamila?”
“Adela, sasa waweza kwenda! Lakini sehemu ninayotaka uende ni barabara ya kuelekea Chalinze. Kuna maiti inasafirishwa ndani ya daladala inatokea Dar es salaam inaelekea Sumbawanga ineku wenzangu wameishuhudia na tena nasikia ni ya kiume.Changamkia! .Jitahidi uiwahi ili upunguze idadi ya maiti ulizolala nazo.Sawa Adela?”
“Sawa baba nimekuelewa!”
Nikauchukuwa ungo nakuweka pembeni yangu.Ulikuwa umewekwa nguvu zetu zote za kutukinga na uchawi.Mkono mmoja nikashikilia mkia na mwingine nikashikilia kibuyu. Nikaingia ndani ya ungo kisha nikaupepea ule mkia hewani kuonesha ishara kuwa nataka kuondoka. Nikapaa! Safari ya kufukuzia maiti barabara iendayo Chalinze ikaanza.
************
***** LIKE na SHARE nyingi zinasaidia kuifanya simulizi hii inoge na kuwa tamu zaidi. Gonga LIKE yako na SHARE simulizi hii.
***** Je Adela atafanikiwa kuona daladala iliyobeba maiti iendayo Sumbawanga? Nini hatma yake kiuchawi?
Tags
HADITHI NA RIWAYA