Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA WILAYA YA KILWA AKAGUA KAZI YA UJENZI WA MKUZA WA BOMBA LA GESI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abadalah Ulega akipata maelezo ya ujenzi wa Mkuza wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam toka kwa Eng...

IMG_3239Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abadalah Ulega akipata maelezo ya
ujenzi wa Mkuza wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam toka kwa Eng Ahmeid Chinemba, Mratibu wa Mradi Mkoa wa Lindi alipokagua kazi zinavyoendelea.
DSC_0478Kambi ya Njia nne wilayani Kilwa ni Moja kati ya kambi za
Wachina Watakaoanza kutandaza bomba la kusafirisha Gesi kati ya
Songosongo,Mtwara kuelekea Dar Zikiwa katika hatua ya umaliziaji wa majengo ya kuishi wafanyakazi..Kambi kama hii ipo katika kijiji cha
Nangurukuru na Kitomanga wilayani Lindi
DSC_0443Baadhi ya askari wa jeshi la Polisi wanaolinda kambi ya Njia nne
wakisiliza maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdalah Ulega
alipokuwa akiwaasa kufuata maadili ya kazi zao hapo kijijini huku
akieleza kusikitishwa kwake kufuatia wizi uliotokea kwa Wachina wa
kambi hiyo
IMG_3320Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdalah Ulega akisikiliza maelezo toka
kwa Mratibu wa mradi huo,Eng Ahmeid Chinemba alipokuwa akikagua kazi zinavyoendelea za kuandaa njia ya litakapopita Bomba la gesi kuanzia vijiji vya somanga hadi Kiranjeranje wilayani Kilwa
DSC_0500Vitanda

Na Abdulaziz Video,Kilwa
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega amefanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya Ujenzi wa njia ya bomba la
gesi(Mkuza)kazi ambayo imeanza kati ya Songosongo,Mtwara Dar na
kutarajiwa kazi zote kukamilika ndani ya Miezi 18

Ulega alitembelea kati ya kijiji cha Somanga na Kiranjeranje kukagua
kazi inavyoendelea na changamoto za na kuzungumza na wananchi na
kuwataka waitumie vyema fursa hiyo katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji ili wanufaike na huduma za kimaendeleo katika wilaya yetu

“Ndg zangu wana kilwa hizi fursa mzitumie kwa kusomesha watoto wenu ili wanufaike na ajira za gesi hii,Hata hivyo nasikitika kwa kuwa
nimeambiwa na hawa wachina kuwa mmeanza kuwaibia jamani tutafika mlikuwa kwa amani na hawa wageni mnapata ajira za muda mnalipwa sasa angalieni tumewaletea askari nyie wenyewe mnaona raha?
Serikali imejipanga na kusimamia mnanufaika na miradi hii…alimalizia Ulega

alipokuwa akisalimiana na wananchi wa njia nne wilayani Kilwa
Kwa Upande wake mratibu wa Mradi huo wa Mkuza Mkoa wa Lindi, Eng Ahmeid Chinemba akitoa maelezo ya kazi hizo kwa Mkuu wa wilaya huyo, Alibainisha kuwa kazi hiyo ambayo Itagharimu Jumla ya Dola Bilion 1.2 inatekelezwa na kampuni ya mabomba ya petrol ya China imeanza kwa kuandaa mkuza kati ya Songosongo Nyamwage kuelekea Dar es salaam na Somanga Nangurukuru Mtwara.

Chinemba pia alieleza kuwa sambamba na ukamilishaji wa mkuza huo pia tayari kambi kuu 3 za za malazi na ofisi kwa wafanyakazi wa kazi hizo zipo katika hatua ya mwisho katika Vijiji vya Njianne, Nangurukuru na Kitomanga ambapo pia mabomba ya kazi yakiwa yanapokelewa katika kambi ya Kiranjeranje

Kufuatia Uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilayani Kilwa na
kusafirishwa kwenda Dar tayari inauzwa kwa zaidi ya Viwanda 30, huku jamii ya wakazi kijiji cha Songosongo wakinufaika na utumiaji wa
nishati ya umeme bila malipo huku Halmashauri ya wilaya Kilwa
ikikusanya kodi ya Huduma pamoja kusaidia huduma mbalimbali za kijamii

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top