Unknown Unknown Author
Title: MWAMUZI WA MPIRA AVULIWA NGUO NA APIGWA HADI KULAZWA HOSPITALI RUKWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NA Walter Mguluchuma, sumbawanga. Mwamuzi na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelazwa kwenye ...

clip_image001NA Walter Mguluchuma, sumbawanga.

Mwamuzi na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelazwa kwenye kituo cha Afya cha Laela baada kushambuliwa na kwa kupigwa sehemu mbalimbali za miili yao katika mchezo wa Ligi ya ujirani mwema.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Kisalala kata ya Laela Mwamuzi wa mchezo huo Eliaza Simzokwe alishambuliwa dk 75 pale alipovamiwa na kundi la mashabiki timu ya Serengeti na kumvua nguo zake kisha kuanza kumpiga hadi kujisaidia haja kubwa wakipinga bao lililofungwa na mchezaji wa timu Muchiza FC, Siyaye Mgonde wakidai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Meneja wa Timu ya Serengeti FC ya Kisalala , Andrew William alisema kuwa baada ya mwamuzi huyo kuvuliwa nguo na kupata kipigo hicho ilibidi baadhi ya wananchi kuingilia kati na kumwokoa hatimaye mwanamke mmoja alimsaidia kwa kumfunga khanga ya kumsitili kabla kukimbizwa kituo cha Afya cha Laela kwa ajili ya matibabu ya majereha mbalimbali kwenye mwili wake.

Baada ya kuona Mwamuzi huyo anazidi kushambauliwa ndipo wachezaji na mashabiki wa timu pinzani ya Muchiza FC waliamua kuingilia kati na kuanza kushambuliana wapinzani wao hali iliyosababisha wachezaji wawili na kocha watimu ya Serengeti kujeruhiwa na kulazwa kwenye kituo hicho cha Afya.

Ugomvi huo ambao ulihatarisha maisha ya washabiki na wachezaji hao ilisababisha kuharibiwa vibaya kwa vyombo vyao vya usafiri ikiwa ni pamoja na pikipiki na baiskeli 10.

Hatahivyo wakati washabiki wa timu ya Serengeti wakidhani kuwa ugomvi huo umeishia hapo lakini usiku mashabiki wa timu jirani ya Muchiza FC kutoka kijiji cha Kitete walikuja tena kuanza kuwasaka wachezaji na washabiki wa timu ya Serengeti nyumba kwa nyumba na kuwashambulia kwa silaha za jadi ikiwa ni pamoja na mikuki na mapanga.

Katika ugomvi huo wa usiku huo, mchezaji wa timu ya Serengeti FC Peter Willy alijeruhiwa kwa kupigwa panga kichwani.

Kufuatia hali hiyo uongozi wa Chama cha soka wilayani Sumbawanga (SURUFA)kimewatahadharisha washabiki wa mchezo huo kuachana na vitendo vya vurugu kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashambulia waamuzi wa mchezo kwa kuwapiga pale wanapochezesha michezo mbalimbali.

Katibu wa SURUFA, Kanyiki Nsokolo alisema kitendo kilichofanya na mashabiki hao ni cha kihuni na hakifai kutokea sehemu zingine.

Alisema kufanyika kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kuendesha masuala ya soka kienyeji pasipo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja mashindano hayo kufanywa pasipo kukishirikisha chama cha soka cha wilaya sanjari kutokuwapo kwa makocha na waamuzi wenye sifa kwaajili ya kucheza michezo mbalimbali ya soka.

SOURCE: Habari na Blogs za Mikoa Tanzania

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top