Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI AFUNGUA WARSHA YA UHIFADHI MISITU, ILIYOENDESHWA NA SHIRIKA LA MPINGO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akifungua warsha ya wadau wa Shirika la Mpingo iliyofanyika katika ukumbi wa PEC(Kwa Sultan) kulia...

RCMkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akifungua warsha
ya wadau wa Shirika la Mpingo iliyofanyika katika ukumbi wa PEC(Kwa Sultan) kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Mpingo, Felician Kilahama na Mkurugenzi wa MCDI,Gasper Makala
MPINGO 1Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa shirika la Mpingo waliohudhuria warsha ya wadau wa Shirika hilo iliyofanyika wilayani kilwa
MPINGO 2Wadau wakisikiliza hotuba ya Ufunguzi wa warsha hiyoKILAHAMAMwenyekiti wa Bodi ya shirika la Mpingo,Felician Kilahama akiongea na wadau wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa lindi kufungua warsha hiyo,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa lindi, mkuu wa wilaya ya kilwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya kilwa ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ally Mohamed MtopaIMG_2935Wajumbe wa bodi na wadau wa shirika la Mpingo wakiwa katika warsha hiyo

Na Abdulaziz Video,kilwa
Mkuu wa mkoa Lindi Ludovick Mwananzilah ameiomba serikali kupitia
wizara ya nishati na madini kupunguza bei ya bidhaa na vifaa vinavyo
tumia mafuta na gesi ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira
unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Ombi hilo amelitolewa kwenye warsha shirikishi ya wadau wa shirika la kuhifadhi mipingo na maendeleo(MCDI) iliyoshirikisha wilaya za Kilwa, Nachingwea na Rufiji iliyofanyika kwenye ukumbi PEC wilayani Kilwa.

Mwanazilah alisema kuharibifu wa mazingira unatokana na kukatwa kwa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa makubwa kutokana na kipato cha wananchi kuwa kidogo ambacho hakiwezi kukidhi kununua mafuta na gasi.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema wizara kwa kushirikiana na
wadau wengine wa mazingira kuhakikisha kuwa bei ya vifaa za gasi
iliyoanza kuzalishwa wilayani Kilwa mkoani Lindi vinapunguzwa bei ili
kuwafanya wananchi wengi wenye kipato kidogo wanaweza kumudu kupata gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kupunguza matumizi ya mkaa na kuni kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

“Ndugu wana warsha, leo hii tumepata fursa ya kukutana na kujadiliana juu ya suala zima la Utunzaji Misitu kiendelevu, Lengo la Warsha hii ni kujadili kwa kina na kukubaliana ni jinsi gani Shirika la MCDI liendelee kuziwezesha jamii katika kusimamia Misitu ya vijiji kwa uendelevu ili Misitu iendelee kuchangia katika kuboresha
maisha ya wananchi wetu”
alisema mkuu huyo wa mkoa.

Alisema ni jambo jema sana kwani Misitu yetu ipo hatarini kuangamia
iwapo haitasimamiwa vizuri na kwa uendelevu. Misitu yetu inakabiliwa
na changamoto nyingi sana ikiwemo kilimo cha kuhamahama na uchomaji moto Misitu.

Mkuu wa mkoa huyo alichukua nafsi hiyo washiriki wote tuzingatie
Usimamizi Bora wa Mazingira na hususani Misitu ili isipotee na
tuendelee kunufaika na manufaa yatokanayo na rasilimali za Misitu
ikiwa ni pamoja na mbao, asali na uuzaji wa hewa ya ukaa. (Carbon).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top