REPORT YA DAKTARI WA MUHIMBILI JUU YA JERAHA LA SHEIKH PONDA LIMESABABISHWA NA NINI.....

clip_image001SHEIKH PONDA AKIWA HOSPITALI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAJERAHA YA SHEIK PONDA ISA PONDA
dar es salaam  12/8/2013

sheikh ponda issa ponda (54) alipokelewa hapa ytaasisi ya ya tiba ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI jana tarehe 11/8/2013 saa 7.30 adhuhuri akitokea hospitali ya taifa muhimbili
baada ya kupokelewa alionekana akiwa na majeraha chini ya
bega la mkono wa kulia lililokuwa limeshonwa mbele na nyuma
madaktari wetu walifanya uchunguzi na kushauri afanyiwe kipimo cha x-ray ili ubaini kama kuna mvunjiko kwenye sehemu ya jeraha
tathimini ya madactari baada ya kupata majibu ya x/ray ilionyesha alikuwa na mvunjiko bila mifupa kupishana.

Vivyo hivyo kidonda hakikuwa katika hali nzuri licha ya tiba ya mwanzo na iliamuliwa afanyiwe upasuaji mpya ili kuzuia maambukizi kama kingeachwa hivyo 
KWA HIYO ....

1-kufwatana na tiba ya awali aliyopata ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla ya kufikishwa moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha lilisababishwa na kitu gani

2-kipimo cha x-ray kilionyesha kwamba alikuwa amepata mvunjiko wa mfupa mkubwa wa bega bila mifupa kupishana

3-hivyo basi sheikh ponda issa ponda anaendelea n matibabu baada ya upasuaji .

Mkurugenzi mtendaji
                   Taasisi ya mifupa na upasuaji wa mishipa ya fahamu MOI

SOURCE:HABARIZUTULEO

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post