JK AAPISHA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU IKULU DAR ES SALAAM LEO

clip_image001Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba (kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Manaibu Katibu wakuu mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu hao Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa tarehe 23 Agosti, 2013, katika viwanja vya Ikulu, amewaapisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu.

Ifuatayo ni Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa leo.

1.    MAKATIBU WAKUU

Ndugu Sophia Elias Kaduma

Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Jumanne Abdallah Sagini

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Uledi Abbas Mussa

Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara

Dr.  Patrick James Makungu

Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Ndugu Alphayo Japani Kidata

Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Ndugu Charles Amos Pallangyo

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Ndugu Sihaba Said Nkinga

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Anna Tayari Maembe

Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

2.    NAIBU MAKATIBU WAKUU

Ndugu Dorothy Stanley Mwanyika

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Fedha za Nje na Madeni)

Ndugu Consolata Philipo Mgimba

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Eng.  Angelina Elias Augustine Madete

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais

Dr. Deodatus Michael Mtasiwa

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - AFYA

Ndugu Monica Lyander Mwamunyange

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi

Ndugu Regina Lucian Kikuli

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu

Ndugu Kagyabukama Edwin Kiliba

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI)

Ndugu Zuberi Mhina Samataba

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) - ELIMU

Dr. Yamungu Kayandabila

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (SERA)

Ndugu Mwitango Rose Shelukindo

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Selassie David Mayunga

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Elisante Ole Gabriel Laizer

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amantius Casmiri Msole

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu

Dar es Salaam.

23 Agosti, 2013

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post