Mwenyekiti wa CCM Taifa akiwasili kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM Dodoma,tayari kwa ufunguzi wa baraza la ushauri la Wazee wa Chama,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma ndugu Adam Kimbisa.

Wasanii wa Kundi la Kyela Beats wakitumbuiza wakati wa sherehe za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, leo Agosti 24,2013.
Katibu wa CCM Taifa ,Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za utangulizi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la CCM.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu pamoja na wanachama wa CCM wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wa Chama wanaounda Baraza la Ushauri la Wazee wa Chama.
Source: CCM Blog