Unknown Unknown Author
Title: REKODI: BALE KUMPIKU CRISTIANO RONALDO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MADRID, HISPANIA REAL Madrid sasa imeamua.  Inataka kuishtua dunia kama ilivyofanya kwa Zinedine Zidane na baadaye Cristiano Ronaldo. Kwa m...

clip_image001MADRID, HISPANIA

REAL Madrid sasa imeamua.  Inataka kuishtua dunia kama ilivyofanya kwa Zinedine Zidane na baadaye Cristiano Ronaldo. Kwa mara nyingine tena inataka kuvunja rekodi ya uhamisho wa dunia kwa kumchukua Gareth Bale kwa kiasi cha Pauni 95 milioni.

Rais wa Madrid, Fiorentino Perez, ambaye ameambatana na timu yake katika ziara ya Marekani, anataka kuhakikisha anatoa kiasi hicho cha pesa na kumchukua Bale kabla kurudi Hispania Agosti 11.

Awali, Madrid ilipeleka ofa ya Pauni 81 milioni kwa ajili ya Bale, lakini ofa hiyo ilikataliwa hapo hapo na Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy ambaye anaamini kuwa Bale ana thamani ya Pauni 100 milioni.

Lakini sasa, Perez ambaye ameambatana na Madrid katika Miji ya Los Angeles, Phoenix, Washington na Miami anatazamiwa kutoa kitita cha Pauni 51 milioni pamoja na kuipa Spurs wachezaji wawili, Angel Di Maria na Fabio Coentrao ambao thamani ya pamoja itapelekea dili hilo kuwa la Pauni 95 milioni.

Juzi Jumapili usiku, Levy alikatisha likizo yake na kurudi London kwa ajili ya kuzungumza na Bale ambaye naye pia amerejea London na kikosi cha Spurs wakitokea Hongkong kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya.

Mashabiki wa Real Madrid wamekuwa wakimshinikiza Perez kumchukua Bale ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya mawinga mahiri zaidi duniani kwa kizazi hiki huku akiwa ameiweka Tottenham Hotspurs katika matawi ya juu kutokana na juhudi zake binafsi.

Hata hivyo, hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa Perez kuwakosha mashabiki wa Madrid kwa kuvunja rekodi ya dunia kwa ajili ya mchezaji wanayemtaka.

Mwaka 2001 alivunja rekodi ya uhamisho duniani wakati alipomchukua kiungo wa Juventus, Mfaransa Zinedine Zidane kwa kiasi cha Pauni 54 milioni.

Kama vile haitoshi akavunja tena rekodi ya dunia Julai 2009 kwa kumchukua kiungo mahiri wa AC Milan, Ricardo Kaka aliyemnyakua kwa Pauni 56 milioni.

Saa kadhaa baada ya kumchukua Kaka, Perez alifungua tena pochi kwa kumchukua staa wa Manchester United, Cristiano Ronaldo kwa dau la Pauni 80 milioni ambalo mpaka sasa ni rekodi ya uhamisho duniani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top