PICHA ZA VIDEO YA WEMA SEPETU AKIPIGWA DENDA YAVUJA

clip_image001Video inayomuonesha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidendeka na mwanaume imevuja mtandaoni...
Haikuweza kufahamika mara moja lengo la Wema na mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Aidany ‘kujishoot’ wakifanya vitendo hivyo ila wanaonekana wakiwa katika mazingira ya ki-Mr & Mrs.
 
Aidha, katika video hiyo, Wema anaonekana kutumia nguvu kubwa kumshawishi Aidany amsogezee mdomo lakini mwanaume huyo anasita na hata alipokubali kudendeka hakutoa ushirikiano wa asilimia 100.
Mwanaume fegi mkononi
Katika video hiyo, mwanaume huyo anaonekana kutumia muda mwingi kuvuta sigara yake huku Wema akiwa bize kumpapasa kimahaba.
Ni filamu?
Baada ya video hiyo kunaswa swali lililokuja ni je, ni sehemu ya filamu za mwanadada huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame au ni uhalisi wa mambo!
 
Katika kujua ukweli, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kupitia simu yake ya mkononi lakini mara nyingi imekuwa ikiita bila kupokelewa.
Aidha, mwandishi alichukua hatua ya kwenda nyumbani kwake maeneo ya Kijitonyama jijini Dar lakini alimkosa na hata alipokwenda ofisini kwake hakuweza kumpata.
:::SOURCE::GAZETI LA IJUMAA::::

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post