OFFICIAL: YANGA YAMALIZANA RASMI NA HAMIS KIIZA

clip_image003Sakata la usajili la mshambuliaji Uganda anayekipiga kwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Dar Young African Hamisi Kiiza limefikia tamati rasmi baada ya Yanga na Kiiza kukubaliana kimsingi kuongeza mkataba mpya wa mshambuliaji huyo.
Kwa mujibu wa Hamis Kiiza ambaye nimekutana nae mapema leo ni kwamba anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili kabla hajaondoka kwenda kwao Uganda.
"Tumefikiana na klabu yangu - sasa nitaongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga msimu ujao. Baada ya kumaliza taratibu zote za kusaini mkataba mpya nitarudi nyumbani Uganda mara moja kabla ya kurudi kuja kujiunga rasmi na wenzangu kwenye pre-season," Kiiza alisema.

HABARI KWA HISANI YA SHAFIHDAUDA.COM

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post