Unknown Unknown Author
Title: PENZI LA FEZA KWA ONEAL LAZIDI KUCHANUA,
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kama ulikuwa unahisi kuwa uhusiano wa Feza na Oneal unaishiwa fleva, basi hauko sahihi. Wandani hawa wameendelea kuiimarisha ngome yao ya m...
clip_image002Kama ulikuwa unahisi kuwa uhusiano wa Feza na Oneal unaishiwa fleva, basi hauko sahihi. Wandani hawa wameendelea kuiimarisha ngome yao ya mahaba ili kamwe isije kushambuliwa na wameendelea kupanga mipango ya kuliendeleza penzi lao baada ya The Chase.
“We’re getting more serious,” Feza alimwambia Big Brother.
“Kukutana na Oneal kwenye nyumba hii kumeonesha upande wangu ambao sikudhani watu wangeuona”, alisema Feza.
“Upande wa ulaini na udhaifu wangu. Marafiki zangu nyumbani wanasema nimekuwa rahisi sana na napotea. Mtu mmoja anahitaji kwa kiasi fulani kuwa mjinga kwenye uhusiano. Ni ngumu sana pia, sababu wakati mwingine nataka kuwa mkali na siwezi sababu uhusiano huu si tu unanihusu mimi. Unanihusu mimi Oneal na Africa.”
Feza alimwambia Biggie kuwa yeye na mpenzi wake huyo raia wa Botswana wana hamu kubwa siku wanaondoka mjengoni humo kwenda kuundeleza zaidi uhusiano wao.



About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top