MJI WA LINDI HATARINI KUPATA MAGONJWA YA MATUMBO IKIWEMO KIPINDUPINDU

DSCF9059Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi

Na A bdulaziz Video Lindi
Wakazi wa Manispaa ya Lindi, kwa takribani juma moja sasa,
wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa upatikanaji maji safi na salama na kulazimika kutumia maji ya visima vya kienyeji vilivyochimbwa kwenye baadhi ya makazi ya watu.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mtandao huu kuhusiana na tatizo
hilo, wameonesha hofu yao ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa ya
matumbo ikiwemo kipindupindu kwa vile maji ya visima wanayotumia kwa sasa siyo safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Lindi mjini(LUWASA), Idrisa Sengulo, pamoja na kukiri kuwepo kwa tatizo hilo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mamlaka, amewaomba radhi wananchi kwa tatizo hilo ambalo amesema kama mambo yakienda vizuri linaweza kutatuliwa ktk kipindi cha siku mbili zijazo.

Amesema mahitaji ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Lindi ni lita
milioni 5 kwa siku, ikilinganishwa na lita lita milioni 1,340,000 tu
kwa siku zinazopatikana kwa sasa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post