MAJANGA IMEENIPA DILI NONO LA KUREKODI MOVIE SOUTH ASEMA SNURA

clip_image002Snura Mushi mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi amedai kuwa muziki ulimpa dili ya kwenda kurekodi filamu Afrika ya Kusini, anasema kuwa watayarishaji wa filamu ya Tandeka iliyorekodi jijini Pretoria kwa kuwashirikisha wasanii watanzania waishio Afrika ya Kusini imetokana na kufanya vizuri katika muziki hasa nyimbo yake ya Majanga.

clip_image002[8]Snura Mushi akiwa katika pozi matata.

Filamu kwa sasa inachangamoto sana hilo lilinifanya nirudi katika muziki huku nikichagua filamu za kuigiza na kujikita katika muziki zaidi ambao unanifanya niwe bussy sana, lakini ninachofurahia kupitia nyimbo yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia Afrika kusini pia nilipewa uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”anasema Snura.

clip_image002[10]Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona na kumwita katika usahili aliposhinda alipewa muswada (Script) na kuigiza kama mhusika mkuu ambaye aliigiza kwa umahiri mkubwa filamu ya Tandeka imetumia lugha mbalimbali ikiwa Kiswahili, Kizulu na Kiingereza, Snura ni msanii mwigizaji wa filamu aliyetokea katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post