Umeona dashboard yake ilivyo
Mifano michache ni watu wanaomudu kutengeneza magobole, mashine mbalimbali na vitu vingine na hata wabunifu wa mrusho wa matangazoi ya radio, ambao badala ya kuwezeshwa hupata vikwazo ikiwamo kunaswa na vyombo vya dola na kufunguliwa mashtaka ilihali wangeweza kutumika kuitangaza Tanzania.
Hapo juu ni mmoja wa wabunifu wa Kitanzania aliyeweza kutengeneza gari ambalo alitumia muda wa miezi sita kulikamilisha kwa kuokoteza vifaa na kulipambana kiasilia kwa kutumia malighafi ya misitu.
Majina yake kamili ni Kenneth Joseph Mwang'oka ambaye alikuwa moja ya vivutio katika Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba kwa ubunifu wa gari hilo linalotumia injini ya Toyota na kuongeza ubunifu wao kiasi kwamba gari hilo lililomgharimu kiasi cha Sh Milioni 8.6 kutembea kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Mwenyeji huyo wa mkoa wa Mbeya, lakini ubunifu wake kaufanyia mjini Iringa anasema lengo lake ni kuhakikisha anakuja kuntengeneza vitu zaidi ya gari hilo la aina yake.
Tags
HABARI ZA KITAIFA