HIZO DOZI ZA BAYERN CHINI YA GUARDIOLA USIPIME, YASHINDA MABAO 24 KATIKA MECHI MBILI JANA NA LEO

clip_image002KLABU ya Bayern Munich imefunga bao lake la 24 katika mechi mbili tu ilizocheza chini ya Pep Guardiola kufuatia ushindi wa 9-1 dhidi ya TSV Regen usiku huu katika mchezo wa kirafiki.
Mabingwa hao wa Ulaya walikuwa wanajipima na timu hiyo ya jimboni katika maandalizi ya msimu mpya kusherehekea miaka 125 ya Regen.
Na mabao matatu  ya Julian Green, mawili ya Patrick Weirauch na mengine ya Thomas Mueller, Toni Kroos, Emre Can na Alessandro Schoepf yalitosha kutengeneza ushindi huo mnono.
Katika mchezo huo, wenyeji walitangulia kuishitua Regan kwa bao la dakika ya sita la Daniel Kopp.
Matokeo hayo yanakuja kufuatia ushindi mwingine mnono zaidi wa mabao 15-1 dhidi ya Wildenau jana huo ukiwa mchezo wa kwanza wa Guardiola.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post