BUFFON AOKOA PENALTI TATU IKIWEMO YA FORLAN KUIPA ITALIA USHINDI WA TATU KOMBE MABARA

clip_image001Shujaa: Gianluigi Buffon ameokoa penalti tatu

KIPA Gianluigi Buffon amekuwa shujaa wa Italia usiku huu baada ya kuokoa michomo mitatu ya penalti na kuiwezesha The Azzurri kutwaa nafasi ya tatu katika Kombe la Mabara baada ya kuifunga Uruguay kwa penalti 3-2.

Timu hizo zilitoka sare ya 2-2 baada ya dakika 120 huku Italia wakitengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

Davide Astori aliwafungia Wataliano bao la kuongoza dakika ya 25 kabla ya Edinson Cavani kusawazisha dakika ya 58.

Alessandro Diamanti akaifungia bao la Italia dakika ya 73, kabla ya Cavani kusawazisha tena 78 na mchezo kuhakia katika muda wa nyongeza, ambako ilishuhudiwa Riccardo Montolivo akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Kisha Buffon akaokoa mikwaju ya Diego Forlan, Martin Caceres na Walter Gargano kuipa ushindi Italia.

Alberto Aquilani, Cavani, Stephan El Shaarawy na Suarez wote walifunga kabla ya Mattia De Sciglio kukosa.

Caceres akakosa na Emanuele Giaccherini akafunga kabla ya Buffon kuokoa mkwaju wa Gargano.

Kikosi cha Italia kilikuwa: Buffon, Maggio, Chiellini, Astori/Bonucci dk96, De Sciglio, Candreva, De Rossi/Aquilani dk70, Montolivo, Diamanti/Giaccherini dk82, Gilardino na El Shaarawy.

Uruguay: Muslera, Caceres, Lugano, Maxi Pereira/Pereira dk81, Godin, Gargano, Rodriguez/Gonzalez dk56, Arevalo Rios/Perez dk106, Forlan, Suarez na Cavani.Third place: Italy won the third-place after an entertaining match with UruguayWashindi wa tatu: Italia wakisherehekea kuifunga UruguayNo 1: Buffon saves from ForlanNamba 1: Buffon akiokoa penalti ya kwanza ya Uruguay iliyopigwa na Diego ForlanAnd again: He then saved the effort from Walter GarganoNa tena: Kisha akaokoa ya Walter Gargano

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post