UZEMBE KAMA HUU HUGHARIMU MAISHA YA WATU WASIO NA HATIA, ASKARI WA USALAMA BARARANI MSIWAFUMBIE MACHO HAWA

clip_image001Basi la kampuni ya  Hood lililokuwa  likitoka Tunduma  kernda Dar likijaribu  kulipita lori  katika kona kali  za mlima  KitongaHapa  dereva  wa  basi hilo bila  kujali usalama  wa abiria  wake akiendelea  kutaka  kupenya jambo ambalo ni hatari  zaidiHapa  akiwa katika harakati za  kulipita  Lori hilo Hapa  basi  hilo lenye namba  T 751 AVL likinusurika   kugongana  uso kwa uso la basi la Sumry baada ya  kulazimisha  kulipita  lori katika eneo la mlima  Kitonga  huku kukiwa na  kona kali kiasi cha  basi hilo kutaka  kutumbukia katika korongo la mlima  huo kama  linavyoonekana kushoto, kazi ya  usalama  wa abiria na kudhibiti  uzembe wa madereva kama  hawa katika mlima  Kitonga  lipo  mikononi mwa  askari wa kikosi cha usalama  barabarani mkoa wa Iringa ambao mwaka jana  waliagizwa na mkuu wa kikosi hicho Taifa  Mohamed Mpinga  kuweka askari eneo hilo  ila wameonyesha  kupuuzia.

PICHA KWA HISANI YA RICHARD-MWAIKENDA BLOG

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post