Unknown Unknown Author
Title: RIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA PILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RIWAYA: SITAISAHAU facebook MTUNZI: EMMY JOHN Pearson SIMU: 0654 960040 SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA. MAWASILIANO baina ya Dokta Davis na Isab...

clip_image001RIWAYA: SITAISAHAU facebook
MTUNZI: EMMY JOHN Pearson
SIMU: 0654 960040

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA.
MAWASILIANO baina ya Dokta Davis na Isabela katika mtandao
“Unaweza kuvuna hadi milioni mbili…si lazima iwe mwisho wa mwezi!!!.” Ujumbe wake ulisema. Mh!! Macho yakanitoka, nikaingiwa na dharau kabla ya kuendelea na mazungumzo hayo.
“Kivipi??” nilimuuliza ilimradi tu..
“Kirahisi sana.” Alijibu. Sikuridhika na jibu lile nikambambika maswali mfululizo hatimaye Davis akanitumia kwa kirefu ni biashara gani hiyo aliyotaka kufanya nami na kwanini anichague mimi.
Baada ya dakika mbili nilikuwa nimemaliza kuusoma ujumbe mrefu wa Dokta Davis. Nilikuwa natetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa katika mwendokasi wa kutisha sana. Macho yalikuwa hayafumbi bali yanaitazama simu yangu!!! Nilikuwa simuoni Dokta Davis lakini nilikuwa katika TAHARUKI!!!!!
SIKUAMINI!!!!!
ENDELEA
(Biashara ya mtandao)
Kilichonishangaza zaidi ni faida iliyoandikwa na Dokta Davis. Sikuipinga lakini mtaji wake haukuonekana kabisa, swali likawa ni biashara gani hii isiyohitaji mtaji lakini ina faida kubwa kiasi hiki??
Nilitaka kumuuliza lakini nikakumbuka kuwa tayari aliita biashara ya mtandao. Huenda hata mtaji wenyewe ni kiasi tu cha kuwa katika mtandao!
Huenda ni hivyo!! Nikaupitisha uamuzi wa kutouliza swali hilo.
Shida zilizokuwa zikinikabili sikutegemea kuwa naweza kumruhusu roho wa kukataa anitawale. Niliufikiria umaridadi niliotamani kuwa nao kila siku, nikawa naishia kuazima nguo za rafiki zangu, nguo ambazo zilinipendeza na kuniweka katika tamaa ya kumiliki zangu mwenyewe!! Ningeanza vipi kukataa pesa yoyte ile ambayo ingejileta mbele yangu!!!
Mara moja nikakubaliana na Davis kuwa naweza kuifanya biashara ya mtandao. Sikutaka hata kidogo kukumbuka kuwa katika biashara huwa kuna faida na hasara. Nilichowaza ni faida tu!! Kwanini niwaze kuhusu hasara wakati shida yangu ni pesa!!
“Lakini tunatakiwa kuonana sasa itakuwaje!!! Au hakuna mkataba?” nilimuhoji kidogo ili name nionekane nafanya mambo yangu kisomi zaidi.
“Keshokutwa kama ukiwa na nafasi njoo unipokee Airport, haitakuwa mbaya kama utakuja na rafiki yako mmoja anayejua kuongea kiingereza kiasi. Maana napenda sana kampani ya watu wengi!! Si unajua tena kukutana wawili peke yetu sio vyema” Alinijibu kwa sauti yake ya kitakatifu, nikaamini kuwa huyu alikuwa mfanyabiashara kweli. Nikajipa matumaini makubwa huku nikianza kuutukana tena umasikini ambao ni kama nilikuwa nakaribia kuuaga!!
Siku hiyo ikapita nikiwa mpya kabisa kichwani, niliyoyawaza nilijua mimi tu na nafsi yangu.
Wakati nikidhani kuwa nitawasiliana tena na Dokta baada ya siku mbili ambazo alidai kuwa atakuja Tanzania!! Haikuwa hivyo!!
Ilikuwa saa moja jioni. Sikuwa na mpango wowote wa kupata pesa, ujumbe ukaingia kwenye simu yangu.
“Nitumie namba yako ya akaunti kuna kipesa kidogo nataka nikuwekee ili mtumie kama nauli kuja uwanja wa ndege kunipokea.” Nilishangazwa na meseji hiyo kutoka katika namba ambayo hakika haikuwa ya mtandao wa Afrika mashariki. Bila kuuliza nikajibu ujumbe
ule lakini haukuweza kwenda, simu yangu haikuwa na salio la kutosha.
Ni kama vile upande wa pili ulitambua hilo. Simu ikaanza kuita nikapokea kutoka namba ileile ya kigeni. Alikuwa Dokta Davis, nilimtajia namba za akaunti yangu kwa ufasaha. Ilikuwa mara ya kwanza kusikia sauti yake.
Sio siri dakika kumi zilikuwa nyingi sana ukaingia ujumbe kuwa pesa tayari imewekwa. Sikukumbuka kufunga mlango nilikaza mwendo hadi ‘ATM’ nikaiweka kadi yangu huku nikiwa siamini kama ni kweli ama la. Nilikuwa najua ni longolongo za wanaume wa facebook ambao huwa wengi wa ahadi zisizotimilika. Hwakutimizii ahadi mpaka ukubaliane na matakwa yao!!! Mapenzi!!
Akaunti yangu haikuwa na pesa kabisa!! Nikatarajia kuumbuka na kufadhaika iwapo sitakuta pesa.
“Salio lako ni 666,666” macho yalisoma tarakimu hizo, nilitumia mkono wangu kuzihesabu tarakimu moja baada ya nyingine huku nikijiuliza kuwa hiyo ni elfu sitini ama laki sita? Jibu lilikuwa laki sita. Kijasho!! Hakika kilinitoka wanachokiita kijacho chembamba!! Hata kama ungekuwa wewe hapo, yaani sikuwa na senti mara ndani ya dakika kadhaa nina laki nyingi namna ile.
Niliondoka ATM na shilingi laki mbili. Kinyago gani angenibabaisha pale chuoni? Mimi ndio mimi.
Usiku mzima nilikuwa naitafakari pesa na kazi niliyoahidiwa na Dokta Davis. Kisha nikakumbuka kuwa Davis aliniambia niende na mwenzangu mmoja anayejua kiingereza, Nilianza kujiuliza ni nani ambaye anafaa kuwa nami katika msafara wa kwenda kumpokea mtu huyu muhimu, Dokta Davis. Niliwachambua marafiki zangu mmoja baada ya mwingine, hatimaye nikamchagua Mariana. Huyu alikuwa ni rafiki yangu hasa, lakini tatizo kiingereza kilikuwa kinampiga chenga..nikamsikitikia sana kwa kuikosa nafasi hii hadimu kwa uzembe ama vyovyote vile kushindwa kukijua kiingereza. Mwishowe nikamchagua Happy ambaye hatukuwa karibu kivile lakini alikuwa ana vigezo. Vigezo alivyotaka Davis.
MCHEZO RASMI UKAANZIA HAPA
Ndege ilitua muda ambao dokta Davis alikuwa amenieleza kabla, alitupigia simu baada ya kuwa ameshuka na tukafuata maelekezo ya jinsi ya kuonana naye.
Happy alikuwa mkimya sana kwani hakuwa akijua mengi hivyo aliniachia mimi majukumu yote.
Hatimaye tukaonana na Dokta Davis. Kwa jinsi alivyokuwa muonekano wake na sisi basi ilimpasa yeye aje kutupokea sisi na wala si sisi kwenda kumpokea yeye. Lakini ndio hivyo ni sisi tulienda kumpokea yeye.

Lafudhi yake ilikuwa na mchanganyiko wa kiingereza cha Afrika magharibi na Marekani. Alikuwa na mwili mdogo tu usiokuwa na chochote cha kuvutia sana. Hakuonekana kuwa mtu mwenye pesa, vazi lake aina ya suti ya kizamani halikumkaa vizuri, na mkoba alioubeba haukuwa na thamani yoyote. Aibu ikaanza kunishika mbele ya Happy ambaye niliona kabisa alikuwa amemdharau mgeni wangu.
“Happy, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi. Anaitwa Davis!!” Nilimtambulisha Happy kwa Davis bila kumwambia kama tulikutana facebook. Nikamtambulisha na Happy huku tukienda kwenye taksi iliyotuleta.
“Nipeleke hoteli nzuri kabisa.” Alizungumza Dokta. Nami bila kusita nikamuelekeza dereva kwa kiswahili hoteli nzuri ya kifahari. Moyoni nilikuwa na wasiwasi bado kama Dokta Davis atazimudu gharama za hoteli hiyo. Muonekano wake bado ulikuwa kikwazo kwangu. Hakufanania kabisa kumiliki pesa nyingi!!
Nikapiga moyo konde hatimaye tukafika hotelini, upesi upesi nikamlipa dereva wa taksi pesa yake.
Tulipofika ndani ndipo mambo yakaanza na presha iliyokuwa inanipanda ikashuka. Alipolipa kwa mfumo wa dola bili za hoteli alinikata wasiwasi wangu!!!

Hapo kabla nilikuwa sijawahi kuingia hoteli yenye hadhi kama ile. Nilikuwa nashangaa shangaa tu pale ndani, sikujua ni wapi mlango unafunguliwa, sikuona mahali pa kuwashia taa baada ya kuingia ndani, na ilinishtua kengele iliyopiga kelele baada ya kuwa mlango haujafungwa vizuri. Hata Happy naye nilimwona akishangaa shangaa, lakini Davis alionekana mzoefu sana wa sehemu kama hizi. Heshima ikaanza kujengeka, kimoyomoyo nikamuomba msamaha kwa kumuona yeye kama mshamba. Washamba tulikuwa sisi.
Tulizungumza mengi sana na Davis, alitawala maongezi kutokana na maswali aliyokuwa anatuuliza. Tulimweleza maisha magumu tunayopitia pale chuoni. Alisikitika sana na kuulaani umasikini.
“Nimewahi kuwa masikini, nimeishi maisha ya kimasikini na hata mama yangu anakufa mimi nikiwa masikini bado. Nyinyi bado vijana na kama mama zenu wanaishi basi hakikisheni hawafi wakisikitika kuwa ninyi ni masikini. Mama alifanya wajibu wa kukuzaeni ninyi lakini anatakiwa kulipwa kwa wema huo. Sio afe akinung’unika” alizungumza kwa kiingereza chake kile kile kilichoeleweka vyema. Sauti yake ilifanania na ya wachungaji wa kanisani.
Alikuwa mpole sana!!
Mwanaume sahihi kabisa!! nilijiwazia
****
Siku hiyo alitupatia shilingi laki moja kwa ajili ya nauli za kurudi chuoni kila mmoja ya kwake. Happy alipagawa nayo kila mara alirudia kusema asante huku Davis akimwambia asijali ni hali ya kawaida. Davis wa maajabu hakuulizia kabisa juu ya ile laki sita na elfu sitini na sita aliyokuwa ameituma siku mbili nyuma. Na ni afadhali hakuuliza maana nilikuwa sijamshirikisha lolote Happy, hivyo kama angeuliza basi angeniumbua haswa!!
Nikaipokea ile laki moja kinyenyekevu!!
Nikapiga mahesabu kichwani, nilikuwa na jumla ya shilingi zaidi ya laki tano.
Isabela mimi nani wa kunitetemesha!!
Nilipofika hosteli niliyokuwa ninanishi nilitamani kila mtu
anitambue Isabella nilikuwa nina shilingi ngapi mfukoni na pia wasiache kujua juu ya salio lililokuwa katika akaunti yangu. Nilifika ndani na kujibweteka huku nikijisikia mwanamke mwenye bahati kupita wote. Nani wa kunisumbua!!

Nilimkumbuka John Paul, huyu alikuwa ni mpenzi wangu ambaye licha ya kuachana bado nilikuwa nampenda. John aliniacha kisa sikuwa na pesa, aliniacha kwa sababu umasikini ulikuwa damuni mwangu, huenda John alidhani naweza kumwambukiza umasikini, John akaniacha na kuunda uhusiano na msichana wa kitajiri, aliyekuwa anamiliki gari yake mwenyewe na kila mara alibadili nguo za bei ghari. Aliitwa Jesca. Nilitamani sana maisha ya Jesca, na hapo ndipo nikakiri kuwa John yupo sawa kabisa kujihusisha naye.
Niliumizwa sana na hali ile ya kuachwa na John, nilijipa moyo kuwa siku moja nami nitapata bahati ya kupendwa tena. Lakini bahati mbaya kila aliyekuja alionekana kuwa ni mdanganyifu.
Yale matendo ya kejeli aliyonifanyia John, niliamini sio kwa kupenda kwake bali msukumo kutoka kwa Jesca yule binti wa kitajiri.
Hasira ikanipanda maradufu sasa nikauona ule wakati wa kulipiza kisasi ulikuwa umefika.

Wakati wa kumwonyesha John kuwa sasa nina pesa!!! Nikawaza kumiliki gari, nikawaza kuwa mwanadada asiyepitwa na vazi lolote jipya na la kisasa. Na kubwa zaidi nikamuwaza Dokta…..dokta Davis. Mwanaume wa kimataifa!!
Nikamjengea picha kaka huyu iwapo atakuwa mpenzi wangu, kwanza nitakuwa na amri juu ya pesa zake, na pili nitakuwa Mrs. Davis. Lolote analofanya lazima nishirikishwe. Nitamfundisha jinsi ya kuvaa ili awe na mvuto mbele ya watu!! Halafu namfundisha pia mambo ya starehe ili tuwafunike wabaya wangu!!
Mh!! Itawauma kweli Isabella nina mchumba kutoka Marekani. Nilijisemea huku nikitabasamu.
Zile picha za dokta Davis ambazo mwanzoni niliziona kuwa hazina mvuto sasa nikaziona kuwa hazina mfanowe katika utanashati, eti nikaanza kujisemea kuwa hakuna mwanaume kama yeye!! ajabu!! dokta akawa dokta kweli. Uchafu gani mwingine wa kunisumbua humo facebook?? Nilijiuliza. Kisha nikagundua nilianza kujengeka kiburi kichwani!!!

Usingizi ulinipitia nikaja kushtuka saa kumi na mbili asubuhi.
Ni kama niliamka wakati sahihi. Dokta akapiga simu kwa namba mpya ya Tranzania ambayo aliinunua siku iliyopita.
“Mchukue gari ya kukodi, mwambie dereva tutamtumia siku
nzima.” Alitoa maelekezo hayo Davis. Nikafuata maelekezo kwa kiherehere. Ni kama tayari alikuwa wangu maana kila kitu alinishirikisha mimi.
Baada ya saa zima nilikuwa katika gari la kukodi aina ya Toyota VX. Sikuzionea huruma gharama za kumlipa dereva na gari lake. Kwani mtoa pesa nilikuwa mimi??
Kabla ya kwenda kwa dokta nikaamua kwanza kulipa kisasi, nikamuamuru dereva twende chuo. Bahati ilikuwa upande wangu, ile nashuka kwenye gari kwa mbwembwe zote. Karibia wanafunzi kumi niliosoma nao darasa moja waliniona.
Macho yao yalionyesha kutoamini nami sikuwajali kimachomacho lakini moyoni nilijiona shujaa, nikatoa amri kadhaa kwa dereva ili wajue kuwa mimi ndiye mmiliki.

Nikajizungusha zungusha hapo kisha nikamwamrisha tena dereva, tukaenda kumchukua Happy. Huku nyuma najua niliacha gumzo!!!
Tulipofika nyumbani kwa Happy, Happy hakuwepo!!! Nikajaribu kupiga simu yake, haikupokelewa. Niliwauliza majirani wakadai kuwa alitoka lakini hawajui kama alirudi ama la.
Anachezea bahati huyu!! Nilijisemea.
Nikapanda ndani ya gari. Safari ya kwenda kwa dokta ikafuata, nakumbuka sikufunga kioo cha dirisha langu. Hii ilikuw maksudi kabisa ili kila anayenifahamu aweze kunitambua, na kama mimi nikiwahi kumuona nilijiwahisha kumwamuru dereva aegeshe gari pembeni niweze kumsalimia.
Nikafika nilipoahidiana kukutana na Davis.
Maajabu nilimkuta Happy akiwa amefika tayari!! Alikuwa na dokta wakinisubiri.
Mchomo wa wivu ukanishambulia na kunijeruhi moyoni, nikaanza kuhisi zile ndoto zangu zimeanza kufifishwa. Happy alinisalimia akiwa na tabasamu mwanana. Dokta akiungana naye kutabasamu. Nami nikajilazimisha nikatabasamu!!!

“Kesho nitarejea nyumbani mara moja….kuna dharula imejitokeza. Lakini kitu kimoja nahitaji mfanikiwe kupitia mimi.” Alianza kutueleza dokta, tukiwa ndani ya gari la kukodi. Kisha akaendelea, “Nitarejea hivi punde tu!! Na nikiwa huko nitakuwa nawasaidia, msisite kunieleza lolote nami nitawasaidia, hata mimi kufika hapa nilikuwa nasaidiwa kwa hiyo ni zamu yangu kusaidia.” Aliongea kwa ukarimu mkubwa.
Kwa mahesabu ya harakaharaka zile dola thamani yake ilikuwa milioni sita za kitanzania. Hizo ndizo Dokta alituachia tugawane. Mimi na Happy.

Kwangu mimi ilikuwa kama ndoto ya mchana!!! Lakini pia nikaingiwa na pepo la ubahili na tamaa. nikatamani Happy asingekuwepo ili ile pesa yote iwe yangu!!
Siku iliyofuata dokta huyu wa ajabu akarejea huko anapojua
yeye!! Hakutaka kusindikizwa uwanja wa ndege.

**DOKTA Davis ametoweka huku akiwaachia pesa wasichana hawa wawili…..DAVIS anatoka wapi na ni kipi anataka???
**Kivipi HAPPY amefika kwa Davis kabla ya Isabela!!
**Je , Isabela atatimiza ndoto zake??

bofya LIKE Katika page yetu kama tunaenda sambamba, COMMENT ukiwanacho ama ukionacho, pia ushauri ni muhimu….SHARE iwafikie wengi wajue kwanini Isabela anasema ‘SITAISAHAU facebook;
ITAENDELEA ….USIKOSEEE!!!!!

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top