Bwana Tajiri: Yaya Toure inaaminika kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi Ligi Kuu England
KLABU ya Manchester City imekuwa bora zaidi katika kulip[a vizuri duniani ikizipiku Barcelona na Real Madrid mwaka huu kileleni.
Tangu bilionea Sheikh Mansour aichukue timu hiyo mwaka 2008, City imekuwa maarufu duniani nje na ndani ya Uwanja, huku wastani wa mishahara ya wachezaji wa kikosi cha kwanza inayolipa ikiwa ni kiasi cha Pauni Milioni 5.2 kwa mwaka.
Wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi City kama Yaya Toure, Sergio Aguero na Carlos Tevez ni sehemu ya nyota wanaolipwa vizuri zaidi duniani, na wastani wa mishahara ya wachezaji wote wa timu ya kwanza kwa wiki ikiwa ni Pauni 100,764, ikiwa ni Pauni 7,000 zaidi dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili, timu ya baseball, LA Dodgers.
Uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Sport Ingintelligence’s Global Sports Salaries Survey (GSSS) kwa mwaka 2013, ukihusisha jarida la ESPN, umegundua kuna klabu nyingine mbili zilizomo kwenye timu 12 bora duniani zinazolipa zaidi baada ya City.
Hizo ni wapinzani wakubwa wa City Jijini Manchester, United wanaoshika nafasi ya 12 kwenye orodha hiyo wakiwa wanalipa wastani wa Pauni Milioni 3.9 kwa mwaka (sawa na Pauni 75,423 kwa wiki kwa kila mchezaji) na Chelsea imeporomoka kutoka nafasi ya nne mwaka jana hadi ya nane, ikiwa na wastani wa kulipa Pauni Milioni 4.1 kwa mwaka (sawa na Pauni 78,053 kwa wiki).
Vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona wanashika nafasi ya tatu na nne, zote zikiwa na wastani wa kulipa Pauni Milioni 4.7 kwa mwaka (sawa na Pauni 90,500 kwa wiki).
Barca na Real walikuwa wanashika namba moja na mbili mwaka jana, lakini kuporomoka kwao pia kumechangiwa na kushuka kwa sarafu ya Euro.
Mahela: Frank Lampard na wachezaji wenzake Chelsea wanaingiza Pauni 78,053 kwa wikiFuraha? Wayne Rooney analipwa Pauni 200,000 kwa wiki Manchester United
Timu za Serie A, Milan inashika nafasi ya sita na Inter ya 10 na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich wapo nafasi ya tisa wakiiwakilisha Bundesliga.
Kuna timu tatu za baseball kwenye 12 Bora na moja ya basketball. MLB teams the Dodgers (nafasi ya pili), New York Yankees (nafasi ya tano) na Philadelphia Phillies (nafasi ya 11).
Namba 1: Kobe Bryant wa LA Lakers anaingiza fedha nyingi kila mwaka NBAMtu wa fedha: Adrian Gonzalez wa timu ya baseball ya Los Angeles Dodgers
Ligi maarufu ya mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA katika 12 Bora inawakilishwa na LA Lakers, inayoshika nafasi ya saba. Wastani wa Lakers unakuzwa na nyota wake kama Kobe Bryant, Dwight Howard na Pau Gasol.
Hesabu zilizotumika katika uchunguzi ni za kuanzia msimu wa 2012/2013 katika NBA, NHL na NFL na kwa msimu uliokamilika mwishoni mwa mwaka 2012 katika ligi nyingine.
Taarifa zinahusisha kiwango cha wastani wa mishahara katika Ligi 12 maarufu zaidi duniani (imeegemea kwenye wastani wa mahudhurio).
Ligi hizo ni NFL, Bundesliga, Premier League, AFL, MLB, La Liga, CFL, NPB, Serie A, IPL, NHL na NBA.
Wachezaji wa Bayern Munich wakiwa na Kombe la UlayaNionyeshe Messi: Nyota wa Barcelona wameporomoka kutoka nafasi ya kwanza mwaka janaSupa Staa: Cristiano Ronaldo akipungia mashabiki Uwanja wa Santiago Bernabeu wa Real Madrid
Nafasi (Nafasi ya mwaka jana) | Timu | Mchezo | Wastani malipo ya mwaka kwa Pauni (Wastani malipo ya wiki) | Wastani malipo ya mwaka kwa dola (Wastani malipo ya wiki) |
---|---|---|---|---|
1 (3) | Manchester City | Football | £5,239,750 (£100,764) | $8,059,477 ($154,990) |
2 (69) | Los Angeles Dodgers | Baseball | £4,855,783 (£93,380) | $7,468,882 ($143,632) |
3 (2) | Real Madrid | Football | £4,718,172 (£90, 734) | $7,257,216 ($139,562) |
4 (1) | Barcelona | Football | £4,690,430 ($90,201) | $7,214,545 ($138,741) |
5 (6) | New York Yankees | Baseball | £4,649,188 ($89,407) | $7,151,109 ($137,521) |
6 (7) | Milan | Football | £4,251,111 (£81,752) | $6,538,811 ($125,746) |
7 (5) | LA Lakers | Basketball | £4,090,742 (£78,671) | $6,292,403 ($121,008) |
8 (4) | Chelsea | Football | £4,058,742 (£78,053) | $6,242,919 ($120,056) |
9 (8) | Bayern Munich | Football | £4,000,036 (£76,924) | $6,152,622 ($118,320) |
10 (10) | Inter Milan | Football | £4,000,000 (£76,923) | $6,152,566 ($118,319) |
11 (9) | Philadelphia Phillies | Baseball | £3,982,336 (£76,583) | $6,125,397 ($117,796) |
12 (11) | Manchester United | Football | £3,921,987 (£75,423) | $6,032,572 ($116,011) |
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.