Jumapili hii kura za watazamani hazikutosha kumuokoa mrembo wa Kenya Huddah Monroe na Mganda Denzel na hivyo kulazimika kufungasha mizigo na kurudi makwao. Hii inamaanisha wamezikosa $300,000 na pia wamezikosa siku 83 za kujiachia kwenye jumba hilo.
Wakati Huddaha Monroe yuko kwenye wakati wa majonzi, Tweet ya mpenzi wake wa zamani CMB Prezzo inaonekana kumfuta machozi kwa kiasi flani na kujua kuwa bado yuko upande wake hata wakati ambao ameteleza katika kile alichokuwa akishindania.
Prezzo alitweet kuwashukuru wote waliompigina kura Huddah na pia tweet nyingine ilienda kwa mrembo huyo. “A big thanks to all who supported our rep, Huddah, in the on-going BBA game. Africa decided.”
Na hii ilienda kwa Monroe, “Congratulations @huddahmonroe 254 is proud of u. Regardless to ur eviction, know tht ur a STAR! God Bless.”
Wakenya wengi wametweet kumpa moyo Huddah ili asijisikie kama ameshindwa, hii ni moja kati ya tweet za kumtia moyo, “@kennzuxxo: they ad to eliminate you in fear of competition @HUDDAHMONROE".”
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.