Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizindua Kitabu cha Biblia kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kimwera
Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislam wametakiwa kutumia vema
nyadhifa na fursa walizonazo katika kuhakikisha kuwa waumini wao
wanadumisha Amani na Utulivu Nchini ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha waumini wao bila kujali mipasuko mbalimbali inayojitokeza Hapa NchiniWito huo Umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe Mara baada ya Misa iliyoambatana na Uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hosteli ya kanisa katoliki parokia ya Nachingwea sambamba na uzinduzi wa Kitabu cha maandiko yasehemu ya bibilia iliyotafsiliwa kwa lugha ya kabila la KimweraMembe alibainisha kuwa hali inayojitokeza hivi sasa inaweza kukomeshwa iwapo viongozi wa dini watakuwa msitari wa mbele kuwaelimisha waumini wao madhara ya ukosefu wa amani na Kutokubali kurubuniwa na kuwa Vyanzo vya Uvunjifu wa Amani.Awali akisoma taarifa ya Umoja wa Makanisa ya kikristo
Nachingwea, Mchungaji wa EAGT, Pius Mnombela alieleza kuwa Umoja huo umefanikiwa kutafsiri vitabu vyote vya agano jipya ambapo vitabu vya Injili ya Luka na Marko vimefanyiwa ukaguzi wa awali na kubainisha lengo la kuanzisha Mpango wa Kuanzisha Utafsri huo na uzinduzi wa kitabu cha Biblia kwa Lugha Asili ya KimweraAkiongea na mwandishi wa Mtandao huu kuhusiana na Shughuli hizo hizo katika Parokia ya Nachingwea, Fr Ngombo Aliwataka waumini kuchangia Parokia zao kufuatia Makanisa Mengi kukosa wafadhili wa Nje ambapo katika Harambee Iliyoendeshwa na Waziri Membe na kufanikisha kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni 31 kati ya fedha hizo Waziri huyo alichangia shilingi milioni 10 pia aliahidi kuhakikisha Jengo
hilo linakamilika kama lilivyokusudiwa kufuatia Nguvu kubwa
zilizoonyeshwa na waumini mbalimbaliUzinduzi huo wa Biblia ya Kimwera,Uwekaji wa Jiwe la Msingi na
Harambee ya kukamilisha ujenzi wa Hostel ya Parokia hiyo umefanikiwa kushirikisha makundi mbalimbali bila kujali Itikadi zao za imani na udhehebu na kuwezesha kupata Tafsiri sahihi ya Biblia kwa Lugha ya Kimwera lugha ambayo utumika na wakazi wengi wa Wilaya za Ruangwa,Lindi na Nachingwea Mkoani LINDI
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.