Unknown Unknown Author
Title: WASANII WAAIRISHA SHOW ZAO KWA AJILI YA MSIBA WA ALBERT NGWEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwemo Mwana Fa, Izzo  Business, pamoja na Kara Pina wamehairisha shoo zao ambazo ziliku...

clip_image001Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwemo Mwana Fa, Izzo  Business, pamoja na Kara Pina wamehairisha shoo zao ambazo zilikuwa zinatarajia kufanyika Mei 31 mwaka huu kwa sababu ya kifo cha msanii mwenzao Albert Mangwea kilichotokea jana nchini Afrika ya Kusini.
Mwana Fa ambaye alitarajia kufanya onyesho lake alilolipa jina la The Finest mwishoni mwa wiki hii amejikuta akiahirisha shoo hiyo kwa sababu ya msiba wa msanii mwenzao

Hii ni moja ya tweet ya kalapina:

Tumepata msiba mkubwa wa msanii mwenzetu ngwear kwa nawaomba radhi funz wote kuwa tumeiharisha show yetu ya tarehe 31 msasani club mpaka ntakapowatangazia mda huu 2naomboleza

Kwa upande wake Izzo Business alieleza  sababu ya kuahirisha shoo hiyo, alisema kuwa hawezi kuendelea na ratiba ya shoo hiyo wakati yupo katika wakati wa majonzi kwa kumpoteza msanii wao ambaye pia ni rafiki yao mpendwa .clip_image001[6]Rapper kutoka kundi la weusi ,Joe Makini ametangaza kutokuachia ngoma yake aliyotarajia kuitoa siku ya tarehe 30, kupitia ukurasa wake wa facebook, Joe amesema amesogeza mbele kuachia ngoma hiyo ikiwa ni pamoja na show aliyokuwa anatarajia kuifanya ndani ya club 71 Tegetaclip_image001[8]Mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.
Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.

Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kusitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.

Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top