MMOJA AFARIKI 3 WAJERUHIWA KATIKA AJALI WILAYANI LINDI



Na Abdulaziz,Lindi
Mtu mmoja alietambuliwa kwa Jina la Sudi Ahmaid Lilah (24) Mkazi wa Kitomanga
wilaya Lindi Amefariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya
gari Isuzu Tipper yenye namba za Usajili T441AMC ajali iliyotokea
kati ya kijiji cha Mkwajuni na Namkongo wilayani humo saa Sita za
Usiku kuamkia leo
Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Kilombilo Eliana Mariki ambalo
lilibeba Tofari kwa ajili ya kupeleka katika ujenzi wa kisima cha Maji
Namkongo tofari ambazo zilitoka katika kijiji cha Mitwero limepata
ajali hiyo na kuporomoka katika bonde na Tofari hizo kuufunika Mwili
wa marehemu alifariki hapohapo Kufuatia taarifa ya awali ya Muuguzi wa zahanati ya Namkongo Bi Regina Blasius na Kuthibitishwa na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga na kueleza kuwa Majeruhi wamefahamika kwa Majina ya Godbless Mgati(21) mkazi wa wailes lindi, Juma Abdulrehman(24)mkazi
wa Ndoro na Hassan Masudi(28) Fundi bomba mkazi wa Makonde
wamefikishwa asubuhi hii na kulazwa kwa Matibabu zaidi katika Hospital ya Rufaa ya Sokoine Mjini Lindi
Hata hivyo alieleza kuwa maiti hiyo ya ajali iliyotambulika kwa jina la Sudi
Ahmaid Lilah (24) ambae alikuwa katika gari hilo kama mchukuzi wa kupakia na kushusha tofari hizo Imehifadhiwa katika Hospital hiyo na kuomba ndugu na jamaa kujitokeza kuitambua pamoja na kuichukua kwa Mazishi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post