Wanajeshi 3 wamekufa ajalini mjini Nachingwea mkoani Lindi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Nachingwea kwenda mkoani Mtwara kupinduka na wengine 23 kujeruhiwa
Habari za siri zinadai kuwa majeruhi wanakimbizwa katika hospitali za Ndanda na Nyangao kwa matibabu. Askari hao walikuwa wanakwenda Mtwara kusaidia kutuliza ghasia
Katika hatua nyingine Watu 45 wanashikiliwa na polisi kwa vurugu za kupinga gesi kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba zilizotokea leo.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara Linus Sinzumwa amesema hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa katika matukio yanayoendelea mjini hapa.
Kauli hiyo ya kamanda Sinzumwa inapingana ya Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mohamedi Kodi aliyethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na wengine wengi kujeruhiwa.
Amesema kwa kiasi kikubwa jeshi lake limefanikiwa kutuliza ghasia na kwamba katika maeneo machache wanaendelea na kudhibiti hali hiyo.
katika hali nyingine isiyotarajiwa mawasiliano ya njia ya tv yawa kitendawili kwani matangazo yanapatikana kwa kusua sua..na kwa sasa mji wa lindi uko giza kuanzia saa 7:30usiku tatizo likiwa halijajulikana nini sababu ya kukatika kwa umeme huo.
MBWA WA POLISI TOKA RUVUMA WAWASILI MTWARA
MBWA wa polisi
kutoka songea mkoani Rvuma wamewasili mkoani Mtwara kuimarisha
ulinzi.
Habari za ndani ya
jeshi la polisi mbwa hao watatumika kukamata watia vurugu.
Iakumbukwa kuwa
tangu saa tano asubuhi mji wa Mtwara ulitawaliwa na milio ya mambomu na bunduki
hadi saa 12 jioni ilipotulia, kwa sasa milio hiyo inaiskika mara chache baada ya
nusu saa
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.